Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Mhe.Gullamhussein S. Kifu akiongozana na kamati ya ulinzi na usalama pamoja na Mkurugenzi mtendaji Wilaya Ndg.Mohamed I. Mavura na timu yake wametembelea shule za Msingi na Sekondari kukagua maendeleo ya ujenzi na ukarabati wa madarasa yanayotarajiwa kuingiza wanafunzi wa darasa la kwanza na kidato cha kwanza.
Shule mbalimbali zilitembelewa ambazo ni Mkupuka,Zimbwini,Dimani,Kinyanya,Mtawanya,Pagae,Msafiri na Mjawa sekondari.
Wakati wa ziara hiyo Mhe.Mkuu wa Wilaya alifurahishwa na kasi kubwa ya ujenzi na ukarabati wa madarasa pamoja na vyoo na kuwapa pongenzi watendaji wote,Wahe.Madiwani,Wenyeviti wa vijiji na vitongoji pamoja na kamati za shule kwa usimamizi mzuri ambao unaendana na kasi kubwa ya maendeleo ya serikali ya awamu ya tano katika kuhakikisha wanachi wanapata huduma bora na kwa wakati.
Aidha,Mhe. Mkuu wa Wilaya aliwaahidi viongozi wa shule kurudi kujiridhisha kama watoto watakuwa wameingia kwenye madarasa hayo siku ya kufungua shule ambayo ni Jan.11,2021.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.