Tarehe 5.12.2022 majira ya saa 4:10 asubuhi hadi saa 06:24 mchanakatika ukumbi wa ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya yakibiti iliyopo kitongoji cha Rumiozi kata kibiti kulifanyika kikao cha kamatiya ushauri ya wilaya(DCC) kilichoongozwa na Mkuu wa Wilaya Meja Edward Gowelena kuhudhuriwa na Mwenyekiti wa Halmashauri, Katibu tawala wa Wilaya, MkurugenziMtendaji ambaye ndiye katibu wa kamati hiyo, Madiwani, baadhi ya wajumbe wakuu, watendaji kata,maafisa tarafa, wakuu wa idara na vitengo, pamoja na wakuu wataasisi.
Lengo la kikao hicho ilikua ni kujadili taarifa mbalimbali zautendaji kazi wa halmashauri na taasisi zote zilizopo ndani ya wilaya yakibiti.
Wajumbe wa kamati hii walipata wasaa wa kujadili na kupitishataarifa hizo ambapo kwa ujumla wake hali ya utendaji kazi wa taasisi hizo ninzuri aidha shughuli za utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika taasisimbalimbali unaendelea.
Vilevile mwenyekiti wa kikao hicho Meja Edward Gowele ameshaurikwamba halmashauri ihakikishe inatenga bajeti kwa ajili ya shughuli za doria nadharula hususani kwa ajili ya migogoro ya wakulima na wafugaji kwani kilimondio uti wa mgongo wa mapato ya wilaya yetu. Na kutokutenga bajeti hiikutapelekea kuzorotesha ufanisi wa shughuli hizo kwani mara nyingi wanafanyashughuli za doria au uokoaji kwa uzalendo wa hali ya juu.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.