23.07. 2024
Kanisa La KKKT-DMP Jimbo la Kusini Misioni ya Kibiti wamekabidhi msaada wa nguo na viatu vilivyotolewa na Washarika mbalimbali kwa wahanga waliokumbwa na Maafa ya Mafuriko Wilayani humo.
Akizungumza wakati akikabidhi vitu hivyo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kibiti, Mchungaji Kiongozi wa Misioni ya Kibiti Mch. KAUNDA KENSE amesema Kanisa litaendelea kushirikiana na Serikali kuhakikisha wananchi wanaendelea kubaki salama.
Aidha, Mkuu wa Wilaya Kibiti Kanali JOSEPH KOLOMBO amelishukuru kanisa hilo kwa msaada waliotoa na kuomba wadau kuendelea kujitokeza kutoa misaada mbalimbali kwa wahitaji pale wanapohitaji.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.