Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti imeungana na watanzania wote nchini kusheherekea miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania bara katika ukumbi wa Ofisi za Halmashauri ambayo nchi nzima yamefanyika katika ngazi ya Wilaya na kusheheneshwa na kauli mbiu ya mwaka isemayo AMANI NA UMOJA NI NGUZO YA MAENDELEO YETU.
Kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Mohamed Mavura, amewapongeza wananchi na watumishi wa ngazi mbalimbali chama na Serikali na viongozi wa dini kwa namna walivyojitokeza kuitikia wito wa kusheherekea miaka 61 Tanzania . Aidha Bwana Mavura ameeleza jinsi ambavyo Serikali imefanya kazi kubwa kwa Halmashauri yetu, ikiwa ni Pamoja na miradi mbalimbali ya maendeleo iliyokamilika na inayoendelea kujengwa katika kada mbalimbali hususani, Elimu, Afya, Miundombinu ya barabara, maji, umeme n.k
Akizungumzia kwa niaba ya Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Meja Edward Gowele ambaye alikuwa mgeni rasmi, Katibu Tawala wa wilaya (DAS) Ndg. Milongo Sanga amesema tangu kupata uhuru kibiti inajivunia kwa kuwa na mafanikio yenye tija katika sekta mbalimbali za kilimo ,viwanda,Elimu,miundo mbinu Afya maji n.k jambo ambalo awali haikuwa rahisi katika maeneo yetu ya kibiti.
Vile vile Sanga amesema Pato la wilaya limeongezeka mara dufu Kutoka Tsh.939,791,435.20 kwa mwaka 2016-17 Hadi kufikia TSH.2,492,877,687.49 kwa mwaka 2021-22 hayo ni mafanikio makubwa ambayo kibiti inajivunia kuyapata ndani ya miaka 61 ya uhuru na tangu kuanzishwa kwa Wilaya ya Kibiti.
Hata hivyo maadhimisho hayo yaliambatana na utoaji wa zawadi ya cheti na fedha taslimu kwa washindi wa uandishi wa Insha kutoka shule za msingi na sekondari ulioanza kushindanishwa tangu tarehe 1/12/2022 kabla ya kilele cha maadhimisho kama ilivyoekezwa na Serikali.
Maadhimisho yaliambatana na watoa mada 6 ambao Kwa nyakati tofauti wameipongeza Serikali Kwa namna inavyohakikisha Tanzania inapata Maendeleo ukilinganisha na kipindi cha nyuma hususani katika Wilaya ya kibiti mafanikio yameonekana katika sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na miundombinu Elimu Afya n.k. bila kusahau uzalendo ambao ni nguzo ya ujenzi wa Taifa .
Vilevile Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Ramadhani Mpendu akizungumza katika sherehe hiyo amewapongeza washiriki wote wa sherehe hiyo wakiwemo watoa mada mbalimbali, viongozi wa Dini na washiriki wote kwa ujumla pia amewataka wakazi wa kibiti na watumishi kwa ujumla kufanya kazi Kwa bidii ili kuendeleza mafanikio yaliyopatikana kwani kibiti kwa Maendeleo inawezekana .
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.