Kwa mara ya kwanza, siku ya mikoko duniani Tanzania imeadhimishwa katika Wilaya ya kibiti katika uwanja wa shule ya Sekondari ya Wavulana Kibiti na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali ambapo shirika la WWF limewezesha kufanyika kwa sherehe hizo.
Lengo la kusheherekea siku hiyo ya mikoko duniani ni kuikumbusha Jamii ya mwambao wa Pwani na na Jamii inayotegemea mazingira ya Pwani, kushirikiana na Serikali, taasisi za mashirika mbalimbali mpaka ngazi ya Taifa kuhifadhi Misitu ya mikoko katika nchi ya Tanzania yenye ukubwa wa hekari 158,000 sawa na 0.4% ya eneo lote la Misitu Tanzania bara hekari mil.48.1.
" Tarehe 26.7. Kila mwaka ilipitishwa kipekee iwe siku ya kusheherekea mikoko ukilinganisha na misitu yote "Alisema Modesta Meddard Msimamizi wa miradi ya Pwani na Bahari
" Tunamshukuru WWF kwa kuona umuhimu na kuchukua fursa ya kikanuni na kisheria kuadhimisha siku ya mikoko kikanda katika wilaya ya Kibiti " Alisema Modesta.
Akizungumzia faida za misitu ya mikoko Bi. Modesta amesema, mikoko ina uwezo wa kupunguza gesi joto(carbon) mara 10 zaidi ya misitu yote na kupunguza hewa ya carbon mara 5 zaidi ya misitu yote mikubwa barani Afrika .
Licha ya eneo la misitu ya mikoko kuwa dogo bado Ina uwezo mkubwa wa kuuza gesi joto aina ya carbon mara 4 zaidi ya misitu mikubwa duniani kama vile misitu ya Amazon
Hata hivyo aliendelea kusema kwamba mikoko huchangia kwa 75% kutengeneza mazalia ya samaki, kuzuia mmomonyoko wa udongo (ardhi) n.k.
Aidha Msimamizi wamiradi kanda ya Pwani na bahari Tanzania amelishukuru shirika la WWF kwa kushirikiana na wanakibiti kwa mara ya kwanza kusheherekea siku hii muhimu ambapo awali walikuwa wakiadhimisha katika Wilaya ya mafia.
" Kusheherekea maadhimisho haya kibiti kutaleta mwamko na shamrashamra kwani wazawa watapata uelewa zaidi wa usimamizi wa mikoko"Alisema Frank Sima (Afisa Mhifadhi Mkuu TFS).
Bw. Sima ameeleza kuwa Moja ya shughuli wanazozifanya ni utunzaji wa mazingira na kuisaidia jamii kujikwamua kiuchumi Kwa kufanya shughuli mbalimbali kupitia vikundi takribani 502 na BMU 271 katika vijiji vya za kibiti.
Vilevile Sima aliongeza kuwa, kiutendaji wanafanya kazi na wilaya 6 kikanda ambazo ni ambazo ni Wilaya ya Kibiti, Mafia, Mkuranga, Rufiji, Kilwa na kigamboni (DSM).
Kipekee Bi. Modesta amesisitiza suala la ushirikiano ili kuweza kuhifadhi Misitu huku akiwapongeza wakala wa huduma za misitu Tanzania TFS kwa kazi nzuri wanazofanya kuhakikisha Uhifadhi unadumu
"Tusipotunza mazingira, tutapoteza samaki waishio baharini na maisha ya wengi wanaotegemea bahari yatakuwa hatarini"Alisema Zakayo Mlenduka mgeni rasmi wa shughuli hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya KIbiti.
Ikumbukwe kuwa, kati ya aina 7 ya mikoko inayopatikana duniani, aina 6 hupatikana katika delta ya Rufiji Wilaya ya Kibiti.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.