14.6.2024
Baraza la Wahe. Madiwani pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo wameendesha harambee na kupata jumla ya Sh.492,000 kwa ajili ya kijana aliyefaulu kujiunga na kidato cha tano katika Shule ya Sekondari ya wavulana Kibiti.
Akiendesha harambee hiyo Diwani wa Kata ya Mtawanya Mhe. Malela Tokha amesema kijana huyo aliyetoka katika Shule ya Sekondari Mtawanya iliyopo Katani kwake amekuwa akifanya vizuri kwenye masomo yake tangu awali. Akiwa kidato cha pili alipata ufaulu wa daraja la kwanza wa alama 7 (“DIV ONE- Point 7”) na kidato cha nne amepata ufaulu wa daraja la kwanza wa alama 9 (“DIV ONE- Point 9”) na amechaguliwa kusoma mchepuo wa Sayansi (PCB).
Kijana Huseni Ali Mpondi anayetoka katika kaya duni na kuelewa na mama yake pekee akiwa na wadogo zake wawili amewashukuru kwa mchango wao kwani utamwezesha kwenda kuanza masomo katika shule aliyochaguliwa.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.