Jumla ya Walimu 123 wanaofundisha darasa la kwanza pamoja na Walimu wa Taaluma wa Shule za Msingi Wilaya ya Kibiti wamepatiwa mafunzo ya somo la kiingereza yenye lengo la kutekeleza mtaala mpya ulioboreshwa kupitia udhamini wa shule Bora chini ya Taasisi ya Elimu Tanzania kwa msaada wa watu wa Ulaya.
Akitoa utambulisho Kaimu Afisa Elimu Mwl. Edwin Kayui aliwasihi Walimu kuzingatia mafunzo wanayopewa ili wakitoka hapo wakawe mabalozi wa kufundisha walimu wenzao ambao hawakupata nafasi hiyo.
Aidha akifungua mafunzo hayo Mgeni rasmi Fredrick Mtaita wa Udhibiti ubora wa Elimu Wilaya ya kibiti alisema lengo la mafunzo ni kuimarisha umahiri wa walimu na Viongozi wa Elimu kwa kutumia mbinu shirikishi za ufundishaji na ujifunzaji wa somo la Kiingereza mashuleni kwa wanafunzi kuanzia darasa la kwanza na kuendelea.
Naye Mwenzeshaji wa mafunzo mwl. Khalid Matiwa amesema, mafunzo hayo yatawawezesha walimu kumudu kuandaa dhana za kufundishia somo hilo sambamba na kuweza kufanya ufuatiliaji wa mtaala huo ambao ni mpya.
Pia Mratibu wa shule Bora Wilaya ya Kibiti Mwl. Violeth Mahimbo amesisitiza kwamba mafunzo hayo yanakwenda kuleta mbinu za kuboresha ufundishaji na ujifunzaji kwa walimu wote wanaofundisha darasa la kwanza na walimu wote kwa ujumla.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.