Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Bw. Hemed Magaro amefungua kikao kazi cha Walimu Wakuu wa shule za sekondari Wilaya ya Kibiti katika ukumbi wa Halmashauri Leo tarehe 20.7.2023 chenye lengo la kujitathmini na kuweka mikakati ya kuinua taaluma pamoja na utekelezaji wa KPI.
Bw. Magaro amewataka Wakuu wa shule kufanya kazi kwa kushirikiana, nidhamu na usimamizi mzuri ili kuweza kupata matokeo chanya kitaaluma.
Hata hivyo amezipongeza shule ya Wama na kayama na shule ya wavulana Kibiti Kwa kufanya vizuri katika mitihani ya kidato Cha 6 huku aliwasisitiza kuongeza bidii kwani upatikanaji wa daraja la l unawezekena.
Vilevile Mkurugenzi Magaro amesisitiza umuhimu wa uwepo wa motisha kwa Walimu hususani wanapofanya vizuri, uwazi wa mapato na matumizi ya fedha kwa kuwashirikisha wazazi na Serikali kupitia ngazi ya Kijiji na Kata jambo linaloleta ufanisi wa kazi kwa uwazi na ari zaidi.
Katika kikao hicho, Afisa Elimu Sekondari Mwl. Anna Shitindi amewataka Wakuu wa shule kuhakikisha wanawasimamia Walimu kikamilifu kuhakikisha wanapata ufaulu wa daraja la l - lll kwa 70% na kuondoa daraja 0 katika shule zote za sekondari Wilayani Kibiti.
"Walimu Wakuu hii ikawe ni agenda ya kudumu katika vikao vyenu kuhakikisha mnatokomeza 0 kwa kidato cha 2 ,4 na 6.
Hata hivyo Shitindi amewaelekeza Wakuu hao wa shule kupitia mikakati waliyojiwekea kuhakikisha wanawatambua na kuwafuatilia wanafunzi wenye uwezo mkubwa na mdogo madarasani kwa kuwasaidia kulingana na uwezo wao ili waweze kufanya vizuri zaidi kupitia masomo mkakati katika michepuo mbalimbali.
" Kuanzia sasa naomba muwatambue wanafunzi kulingana na uwezo wao kwa kuwafuatilia na kuwasaidia ili waweze kufanya vizuri katika mitihani yao na kuepuka daraja 0" Alisema Shitindi.
Pia Shitindi amewaagiza Wakuu shule wa Wilaya ya Kibiti kuongeza kasi ya usimamizi na ufuatiliaji ili kuweza kufikia malengo ambayo Wilaya imejiwekea.
Ili kufikia malengo hayo, Shitindi amewaagiza Wakuu wa shule wote kuhakikisha kwa namna yeyote ile wanadhibiti utoro ambao ni chanzo kikuu cha wanafunzi kupata daraja 0 mashuleni.
Mbali na maelekezo hayo Shitindi ameleekeza kila shule kuhakikisha wanafunzi wa vidato vya mitihani y mwaka huu wanapata chakula cha mchana shuleni ili kuboresha mahudhurio ya wanafunzi shuleni katika kushiriki ujifunzaji.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.