Ni mwaka wa tatu mfululizo Mkoa wa Pwani ukifanya maonesho ya Viwanda na Biashara ambayao yalianza Oktoba 5-10 mwaka huu katika Viwanja vya Maili Moja mjini Kibaha ..
Akiwa katika maonesho hayo ya Viwanda na Biashara Mkoa wa Pwani,Katibu Mkuu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM itikadi na uenezi Mhe. Shaka Hamidu Shaka ameitaka serikali kutoa Elimu na kupima maeneo kwa ajili ya uwekezaji na makazi ikiwa ni sambamba na urasimishaji
Kwa upande kwa migogoro ya Ardhi Mhe. Shaka amesisitiza kuwa kuna kila sababu ya kuwajengea uwezo Wenyeviti wa vijiji,kata na Mitaa ili waweze kufahamu vizuri sheria za Uwekezaji na Ardhi kwa ujumla..
Vilevile Shaka akatoa wito kwa mikoa mingine nchini kutangaza fursa zilizopo katika mikoa yao kwa njia ya maonesho mbalimbali yanayofanyika nchini.
Aidha akampongeza Mhe.Rais Samia Suluhu Hassani hususani katika kuboresha uwekezaji nchini kwa kuinua mwamko mkubwa katika Maonesho haya huku akisisitiza umuhimu wa kuwa na ziara za ukaguzi wa miradi mbalibali inayoendelea nchini.
Maonesho ya Uwekezaji na Biashara Mkoa wa Pwani yalinza mwaka 2020 na mwaka huu yakiwa ni maonesho ya tatu kufanyika na kufana Zaidi huku kauli mbiu ikisema PWANI NI SEHEMU SAHIHI YA UWEKEZAJI.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.