20 . 4. 2024
Kampuni ya Said Salim Bakhresa ya jijini Dar es Salaam (SSB) imeungana na Mbunge wa Jimbo la Kibiti kuwashika mkono waathirika wa Mafuriko yaliyotokea katika Wilaya ya kibiti baada ya mto Rufiji kufurika maji yanayotokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Msaada uliotolewa ni wa mifuko 122 ya unga wa ngano ambapo kila mfuko una vifuko 5 Vyenye ujazo wa kg kumi kumi yenye jumla ya thamani ya fedha za Kitanzania shilingi 9, 930, 800.
Akikabidhi msaada huo Mwakilishi ( dereva) wa Bakhresa ndg.Twaha Mkumba amesema Mkurugenzi ameguswa akaona ni vema kuungana na Mbunge kusaidia waliokumbwa na Mafuriko Wilaya hii ya Kibiti.
Akizungza kwa niaba ya Mbunge Diwani wa Viti Maalum Mhe.Zainab Chitanda ameishukuru Kampuni ya Azam Bakhresa kwa kuwashika mkono wanakibiti waliofikwa na madhira ya Mafuriko sambamba na kumpongeza Mh.Rais kwa juhudi kubwa anazofanya kuwasaidia waathirika wa mafuriko Wilayani Kibiti.
Akipokea msaada huo Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Joseph Kolombo ameishukuru kampuni hiyo kwa msaada huo na ameahidi kwamba msaada utaenda kuwafikia walengwa kama ulivyopokelewa.
Aidha Katibu wa chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kibiti Ndg Zacharia Muhidini akitoa shukrani kwa Kampuni ya Azam Bakhresa baada ya kupokea msaada ameishukuru Serikali ya Dkt. SSH kwa namna inayoendelea kuwashika mkono waathirika hao, uongozi wa Mkoa na Wilaya kwa namna walivyoratibu bila kumsahau Mhe.Twaha Mpembenwe Mbunge wa Jimbo la Kibiti kwa namna anavyokuwa mstari wa mbele kuhakikisha misaada inapatikana.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.