MBUNGE MPEMBENWE ATETA NA WATUMISHI KIBITI.
ASISITIZA UPENDO,USHIRIKIANO NA UVUMILIVU KUWA MIKAKATI MIPYA YA UTENDAJI 2023.
Ikiwa ni siku ya pili ya mwezi wa kwanza 2023 Mbunge wa Jimbo la Kibiti Mhe.Twaha Mpembenwe amekutana na watumishi wa umma wa Halmashauri ya Wilaya kujadili na kuweka mikakati mipya ya kiutendaji Ili kuhakikisha kibiti inasonga mbele.
Akiwa katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo Mhe. Mpembenwe amesisitiza watumishi wote kufanya kazi kwa kushirikiana na kupendana ili kuhakikisha KIBITI inasonga mbele kwani wote ni wajenzi wa nyumba moja hawana budi ya kuwa kitu kimoja.
“Ndugu zangu, watumishi wenzangu, ili tuweze kufanya kazi kwa weledi lazima tupendane na kushrikiana, dumisheni ushirikiano na upendo kazini Jahazi letu litafika salama”alisema Mpembenwe.
Hata Hivyo Mbunge amewataka watumishi kuwa wavumilivu katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwani ni muhimu sana katika utendaji ukizingatia watumishi ni kusayiko la watu kutoka mazingira mbalimbali yenye mila na desturi tofauti.Vumilianeni kwa kuchukuliana madhaifu mpige kazi tunahitaji maendeleo msisikilize maneno yasiyo na tija .
Vilevile ameishukuru halmashauri Kwa ujumla (watumishi na Mkurugenzi) Kwa jinsi wanavyompa ushirikiano kiutendaji jambo linalosaidia kurahisisha kazi zake kwani peke yake isingekuwa rahisi.
“mnanisaidia sana kutekeleza majukumu yangu ya kibunge bila ushirikiano wenu ninyi nisingeweza” alisema Mbunge.
Akijibu maombi ya watumishi Mhe.Twaha amesema ameyapokea na atayafanyika kazi kwa kuyafikisha ngazi husika na mengine kutumia nguvu ya ziada kuyatatua kadri atakavyofanikiwa ikiwa ni pamoja na suala la kukosekana kwa bajeti idara ya ardhi ambayo ilikuwa chini ya Tamisemi na sasa imehamishiwa serikali Kuu .Kwa upande wa marejesho ya mikopo na mafunzo ya watumishi kuongeza utaalam shauri hilo amelibeba pia bila kusahau ajira na makazi ya walimu na kama ilivyokawaida yake Elimu ni kipaumbele cha kwanza na ni ajenda kuu na hivi karibu katika ziara yake ya kikazi jimboni ametoa mifuko 200 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa darasa la Awali (chekechea) litakalowaandaa watoto Kuanza darasa la kwanza katika kitongoji cha Ugenzi Kata ya Mtawanya.
Aidha Mhe. Mpembenwe ameshiriki hafla ya chakula alichokiandaa yeye kwa kula pamoja na watumishi wote wa Halmashauri ikiwa pia ni sehemu ya kusheherekea siku yake ya kuzaliwa ambayo huisheherekea ifikapo tarehe 31 Disemba kila mwaka ikiwa ni sehemu ya shukrani Kwa Mwenyezi Mungu .
Awali Mkurugenzi Mtendaji Mohamed Mavura alimpongeza Mhe.Mbunge kwa ukaribu wake wa kushirikiana na watumishi wa umma kuhakikisha kibiti inaendelea .Vilevile Mavura amewataka watumishi wa umma wakiongozwa na wakuu wa idara kuwa na tabia ya kumshirikisha Mbunge katika masuala mbalimbali ya Wilaya ili aweze kuhudhuria na kutuunganisha na wadau mbalimbali ambao wanaweza kufadhili program zilizopo na kuendelea kupiga hatua Kwa haraka,mbali na hilo Mavura amewataka watumishi hao kumuunga mkono Mbunge huyo ili Kibiti iendelee kupata Maendeleo kwa wakati.
Katika nyakati tofauti Wakuu wa Idara mbalimbali kwa niaba ya watumishi wote, wamempongeza Mhe. Mbunge Twaha Mpembenwe kwa kazi nzuri anazozifanya kwa muda mfupi wa uongozi wake kwani kumekuwa na mabadiliko makubwa ya kimaendeleo hasa katika sekta ya kilimo hususani katika zao la korosho na ufuta,na miradi mbalimbali inayotekekezwa Kwa fedha za mapato ya ndani,Serikali kuu na kutoka kwa wafadhili na mfano mzuri ni ongezeko la vyumba vya madarasa ambao utasaidia watoto kupata Elimu katika maeneo ya karibu bila kusahau huduma za afya Sasa Kuna vituo vya Afya karibia Kila Kata.
Hata hivyo wamesema amekuwa ni MBUNGE wa pekee sana tofauti na maeneo mengine kwa jinsi anavyokuwa karibu na watumishi wa umma na wameahidi pia kushirikiana nae kwa kuhakikisha kibiti inajikwamua kimaendeleo zaidi.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.