24.04.2024.
Wakati Mwenge wa Uhuru ukitarajiwa kupokelewa na kukimbizwa Wilaya ya Kibiti tarehe 6.5.2024, Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Ndg. Rashid Mchatta amekagua baadhi ya miradi itakayopitiwa na Mwenge 2024 Wilayani humo.
Katika ziara hiyo Katibu Tawala huyo aliambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Wataalam kutoka sektetarieti ya Mkoa na Viongozi wa Wilaya ya Kibiti.
Wilayani Kibiti, jumla ya miradi 16 inatarajiwa kukaguliwa na kumulikwa na Mwenge wa Uhuru 2024.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.