29.07.2024
Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti imefanya ziara yake za kawaida ya kutembelea Miradi ya maendeleo iliyotekelezwa ndani ya Halmashauri kwa robo ya nne ya mwaka wa fedha 2023/2024.
Kamati imetembelea miradi 9 iliyopo kwenye hatua mbalimbali ambazo ni Ujenzi, Ukarabati na umaliziaji wa vyumba vya madarasa kwa shule za Msingi 4, Sekondari 3 na Zahanati 2 yenye thamani ya Shilingi 686,021,640.00. Kati ya fedha hizo Shilingi 500,000,000.00 ni kutoka serikali kuu, 109,649,000.00 Mapato ya ndani, 71,372,640.00 fedha kutoka kwa wafadhili ambao ni Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA) na 5,000,000.00 kutoka Mfuko wa Jimbo Kibiti.
Kamati imepongeza Halmashauri kwa kusimamia vyema miradi hiyo huku ikisisitiza Wahandisi kushirikiana kwa ukaribu na mafundi ili kurekebisha dosari zote ndogondogo zilizoonekana.
“Mhandisi, tumeona majengo mengi mmeyasimamia yanaenda vizuri lakini bado kuna changamoto ndogondogo ambazo zinajirudia kwenye miradi mingi jitahidini muwe karibu na mafundi na kuwapa ushauri wa kitaalam ili thamani ya fedha zilizotolewa ionekane” Alisema Mhe. Omary Twanga Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.