Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kibiti anayo furaha kuwajulisha wananchi kuwa Mitihani ya kidato cha nne 2019 itaanza tarehe 04/11/2019
na kidato cha pili itaanza 11/11/2019. Hivyo basi.
1. Anawahimiza vijana wote walio kwenye kambi kuongeza juhudi kwa muda uliobaki.
2. Anawataka vijana wote kuepuka vitendo viovu vya udanganyifu kwenye mitihani kwani kutapelekea kufutwa matokeo yao.
3. Anawatia moyo vijana wote kuwa na utulivu wakati wa mitihani ili kuweza kufanya vizuri.
Mwisho anawatakia kila la kheri watahiniwa wote waweze kuingia kwenye mitihani yao wakiwa na afya njema.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.