04.08.2024
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto Bi. Ikupa Mwasyoge akiwa ameambatana na Afisa Mifugo wa Wilaya hiyo, wametembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti kwenye Maonesho ya 88 katika Viwanja vya Mwl J.K.Nyerere Manispaa ya Morogoro.
Bi. Mwasyoge alipata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali na kupata maelezo katika mabanda yote, kununua baadhi ya bidhaa zilizokuwepo na mwisho akatoa pongezi kwa Uongozi wa Halmshauri ya Kibiti pamoja na wafanyakazi kwa maandalizi mazuri yaliyofanyika.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Chagua Viongozi Bora wa Serikali za mitaa kwa maendeleo endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.