Halmashauri ya wilaya ya kibiti imetenga takribani sh Milion 420 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mapya ya shule za Sekondari ,
Hayo yamesemwa leo na Mohamed I. Mavura (Mwalikwa wa kikao) ambaye ni mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo katika kikao cha Kamati ya maendeleo ya kata ambacho kilifanyika katika ukumbi wa halmashauri huku akiwataka wakandarasi na waratibu elimu kata kufanya uhakiki kabla ya ujenzi kuanza.
Akizungumzia ukuaji wa mji wa kibiti halmashauri imejipanga kufanya uboreshaji wa stendi hiyo ikiwa ni sambamba na kuweka taa kwa ajili ya mwanga wakati wa usiku na kuweka mpangilio mzuri wa wafanyabiashara. Pia amempongeza Diwani wa Kata Hiyo kwa kuwa kaa yake inafanya vizuri katika usimamizi wa miradi ya maendeleo.
Kutokana na kero ya kukatika kwa umeme kwa muda mrefu bila taarifa Ndg. Mavura amesema kunachangia kupunguza mapato ya wananchi ambao biashara zao zinategemea umeme na kuwarudisha nyuma kiuchumi.
Naye Diwani wa kata ya kibiti Ndg. Hamidu Ungando akaomba ufafanuzi kwa Tanesco juu ya gharama za kuunganisha umeme.
Naye Meneja wa TANESCO alisema kuwa kwa maeneo ambayo ni ya vijijini wataendelea kuunganishiwa umeme kwa bei ileile ya awali ya shilingi 27,000/= lakini kwa maeneo yaliyochini ya mamlaka ya mji mdogo wataunganishiwa umeme kwa gharama ya shilingi 321000.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.