Leo 03 Nov, 2023
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mh. Abubakar Kunenge amefanya mkutano na Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri 9 za mkoa wa Pwani ( Chalinze, Bagamoyo, Kibaha mji, Kibaha vijijini, Mkuranga, Kisarawe, Mafia, Rufiji na Kibiti), waandishi pamoja na maafisa wa habari wa taasisi na vyombo mbalimbali katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkurugenzi wa Idara ya Habari – Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Mobhare Matinyi, Wakuu wa wilaya wa Halmashauri za mkoa wa Pwani na wakurugenzi wa taasisi mbalimbali kama TARURA na TANROAD.
Lengo la Mkutano huu likiwa ni kuwapatia wananchi taarifa juu ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita katika mkoa wa Pwani chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Katika Mkutano huo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Bw. Hemed S. Magaro alieleza, Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti ilipokea takribani Sh. Bil. 17.1 kutoka Serikali kuu kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo fedha hizo zilitekeleza yafuatayo : Sh. Mil. 95 kujenga banda la abiria, kizimba cha taka na soko la samaki, Sh. Mil. 471.3 zilitolewa kama mikopo kwa vikundi 132 vya wanawake, vijana na walemavu, Sh. Bil. 6.14 kwenye ujenzi wa Ofisi na nyumba za watumishi, Sh. Bil. 4.46 kutekeleza miradi katika Sekta ya Elimu ya Awali na Msingi na Sh. Bil. 5.93 zilienda katika miradi katika sekta ya Afya.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.