19.06.2024.
Mnada wa pili wa ufuta Mkoa wa Pwani umefanyika katika Wilaya ya Mkuranga kwa njia ya mfumo wa TMX na kufanikiwa kuuza Tani zipatazo 3600.
Katika mnada huo wakulima wote kwa pamoja wamekubaliana kuuza ufuta kwa bei ya wastani ambayo ni sh. 3373.70.
Meneja wa corecu Mkoa wa Pwani Bw. Hamis Mantawela amesema licha ya mauzo hayo kufanyika, takribani Tani 1000 hazikuuzika hivyo wanafanya utaratibu ndani ya wiki hii kuhakikisha zinauzwa kwa njia ya mfumo kadri wazabuni watakavyojitokeza.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Katibu Tarafa wa Mkamba Ndg. Johnson Joachim amewapongeza wakulima kwa kwa kusimamia vyema kilimo na kuhakikisha mazao yanapatikana.
Mbali na pongezi pia amesisitiza vyama vya Msingi kuhakikisha wakulima wote waliofikisha mazao yao ghalani wanalipwa kwa wakati.
Pia amewataka wakulima kutoa ushirikiano, kuwa wavumilivu haswa wakati huu wa mauzo ambapo yanayotumia mfumo, kwani lengo la Serikali ni kuhakikisha kila mkulima anapata haki yake bila usufumbufu.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.