Mwenyekiti na Mgeni rasmi wa kikao cha wadau wa UFUTA Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Joseph Kolombo, ameagiza kufunguliwa kwa maghala yote Wilayani Kibiti, ili wakulima waanze kupeleka ufuta katika kipindi hiki cha msimu ambacho MNADA wa kwanza utafanyika tarehe mosi Juni katika msimu wa kwanza kwa kutumia mfumo wa sanduku la zabuni.
"Wanunuzi wote jitokezeni kununua ufuta kwa kufuata mfumo wa stakabadhi ghalani, kwani unalinda maslahi ya wakulima na wafanyabiashara, kwa kupata bei nzuri na bidhaa zilizo bora kwa wakati" Alisema Kanali Kolombo.
Hayo yamejiri katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti kwenye ufunguzi wa kikao cha wadau wa UFUTA kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kujadili utaratibu wa maandalizi ya mauzo ya ufuta kwa kuzingatia maagizo ya Serikali kwa kutumia mfumo wa stakabadhi ya mazao ghalani.
Vilevile Kanali Kolombo ametoa maelekezo kwa watendaji wa Kata, Wataalam na Viongozi wa vyama vya msingi, kusimamia ukaushwaji na usafirishaji wa UFUTA ili kuhakikisha unakuwa katika hali ya ubora kwa kuhifadhiwa vizuri.
"Watendaji Kata, Wataalam na Viongozi wa vyama vya msingi mkasimamie ukaushwaji na usafirishaji wa UFUTA, ili tuweze kuuza ufuta ulio bora na kujitengenezea masoko" Alisema Kanali Kolombo .
Hata hivyo Mhe. Mkuu wa Wilaya ameviagiza vyama vya msingi kuepuka kupokea, kununua ufuta mchafu na ambao haujakauka huku akiviagiza vyombo vya usalama kuhakikisha vinaweka vizuizi katika njia zote kuhakikisha ufuta hautorishwi kwa manufaa ya kibiti kiuchumi hususani katika maeneo ya Muyuyu hutorosha ufuta na kwenda kuuza ikwiriri nje ya Wilaya. Utaratibu huo unapoteza mapato ndani ya Wilaya na kuzifaidisha Wilaya nyingine.
"Tunapoteza pato la wilaya na kuneemesha wenzentu,uzeni na kununua ufuta wenu Kibiti, Mkurugenzi unda timu ya doria za ila siku, vyombo vya ulinzi na usalama,shirikianeni na Mkurugenzi kuwachulia hatua kali watoroshaji wa UFUTA".
Aidha ameziagiza Taasisi za Benki kuweka mfumo wa kutoa mikopo kwa wakulima, Ili waweze kununua pembejeo kwani ni matarajio ya Wilaya kuzalisha kilo 10,000,000 za ufuta 2021/22. Na ili kufikia malengo hayo, Mkulima peke yake hawezi bila kupata rasilimali fedha.
Kuhusu utoaji wa elimu vijijini, Kanali Kolombo amelipokea na kusema kwamba ni jambo jema, na pindi Wataalam kutoka Tali Naliendele watakapofika wahakikishe wanawasiliana / kuonana na Halmashauri ya Wilaya kabla ya kwenda vijijini.
Akisoma taarifa ya maandalizi minada ya zao la UFUTA ya 2023 Mkurugenzi Mtendaji ndg. Mohamed Mavura amewapongeza wakulima wa kibiti Kwa kupitisha tozo ya sh 20 Kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya elimu.
Mbali na hilo kupitia tozo kwa maendeleo ya Wilaya amezitaka Taasisi mbalimbali zilizopo ndani ya Wilaya, Amcos ,wamiliki wa maghala n.k kuisapoti Wilaya katika miradi ya Maendeleo ikawe ni sehemu ya kuridisha shukrani kwenye Jamii .
Aidha amesema shughuli zinazoendelea kwa Sasa ni kufunguaji wa maghala makuu na vyama vya USHIRIKA vya msingi, kutoa matangazo kwa wakulima kwenye Kata na vijiji kuhakikisha wanakausha na kusafirisha ufuta kupeleka kwenya maghala ya vyama vya USHIRIKA. Mbali na hilo pia shughuli nyingine zinazoendelea ni kuulinda ufuta kwa kufanya doria za kudhibiti utoroshaji wa UFUTA na ununuzi wa kangomba sambamba na kufanyika Kwa ukaguzi wa mzani kwenye maghala ya Amcos. Mkurugenzi Mavura pia amewataka wakulima kuendana na mabadiliko ya Hali ya hewa, yanayopelekea misimu kubadilika kama vile jua Kali kuwaka kuwaka Kwa kipindi kirefu na kusababisha ufuta kukauka mashambani na mvua kuonyesha wakati wa uvunaji.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.