Ofisi ya Rais TAMISEMI kupitia Wizara ya afya kwa kushirikiana na E Fm MUZIKI MNENE imeendesha kampeni ya BEGA KWA BEGA UJANJA KUCHANJA yenye lengo la kuongeza kasi ya chanjo ya uviko 19 kwa hiari katika Mkoa wa Pwani kuanzia Disemba 14-20 mwaka huu.
Tamasha hilo linahusisha wasanii mbalimbali katika kutoa hamasa ya uchanjaji wa chanjo ya uviko 19 katika wilaya zote za mkoa wa PWANI kama ilivyoelekezwa ambapo katika wilaya ya Kibiti kampeni hiyo imefanyika Kata za Kibiti ,Bungu na Mjawa.
Jumla ya watu 3157 wamejitokeza na kupata chanjo ya uviko 19 kati yao wanawake ni 1724 wanaume ni 1433 ambapo katika tamasha hilo wanawake wameongoza kwa idadi kubwa zaidi kujitokeza kuchanja.
Awali, kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Meja Edward Gowele aliwataka wakazi wote wa kibiti ambao hawajapata chanjo wajitokeze KUCHANJA kwani chanjo ni salama haina madhara yeyote. Pia aliwasisitiza wananchi kutoa ushirikiano kwa wanaotoa chanjo mitaani ili kurahisisha huduma hiyo.
Aidha Mganga Mkuu wa Wilaya Elizabeth Oming’o ameipongeza serikali kwa ubunifu wa kutumia wasanii kwani imekuwa ni hamasa kubwa mbali na burdani, huduma imefika kwenye jamii na watu wamechanja. Hata hivyo amefurahishwa na tamasha la MUZIKI mnene ambalo limeshirikisha wasanii na mwitikito umekua ni mkubwa sana Kwa Wilaya ya Kibiti.
Aidha, Oming’o ametoa wito wa kuendelea kutoa elimu na kuhamasisha wananchi wote kwa ujumla wahamasike kuchanja na kuondokana na taarifa za kupotoshwa kwani chanjo hiyo ni salama na haina madhara yeyote.
Akizungumza kwa niaba ya wakazi wa Kibiti Mbegu Abdallah Mzuri amesema wamefurahishwa na uratibu wa huduma hiyo kwani wameelishwa na kuburudishwa kwa wakati mmoja na watu wamechanja ni hamasa iliyovutia sana.
Zoezi hili ni endelevu kwani ugonjwa bado upo na unaua, na hii ni awamu ya pili ya chanjo kwa ufadhili wa shirika la afya duniani Katika mikoa ambayo awali hamasa ilikuwa ndogo na idadi ya watu waliochanja ilikuwa ndogo pia ukiwepo na Mkoa wa PWANI.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.