NBC YAMWAGA MSAADA WA MADAWATI KIBITI
Benki ya NBC leo tarehe 17/04/2021 kwenye ofisi ya mkuu wa Wilaya imekabidhi jumla ya Madawati 250 kwa ajili ya Watoto wa shule za msingi pamoja na viti na meza 250 kwa Watoto wa shule za sekondari kwa Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Mhe.Gulamhussein S.Kifu.Wakizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi mkuu wa NBC Ndg.Elibariki Masuke ambaye ni Mkurugenzi wa wateja wadogowadogo pamoja na Bi.Neema Rose Singo Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano kwa pamoja walikabidhi madawati haya kwa niaba yake na kueleza kuwa ni utaratibu wa kawaida wa Benki yao kutoa misaada mbalimbali kwenye maeneo yenye mahitaji kama Kibiti.Nae Mkuu wa Wilaya alipokea msaada huu mkubwa toka NBC kwa furaha kubwa na kuwaagiza wawakilishi waliotumwa kupeleka shukrani zake za dhati kwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NBC na kumuomba isiwe mwisho wa kutusaidia kwani Wilaya hii ni mpya bado inamahitaji mengi.Baada ya Hafla hii mkuu wa Wilaya alimkabidhi madawati haya mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Kibiti Ndg.Mohamed I. Mavura na kumtaka asambaze madawati haya mashuleni kwa haraka ili yakafanye kazi iliyokusudiwa na pia alisisitiza kuyatunza.
Shukurani nyingi zimfikie Mbunge wa Jimbo la Kibiti Mhe.Twaha A. Mpembenwe kwa jitihada zake za waziwazi za kuwahudumia wananchi wake kwa kufuatilia na kuwashawishi NBC hatimae kutupatia msaada huu mkubwa wenye kuacha alama kubwa kwa jamii ya Kibiti.
Baada ya hafla ya kukabidhi madawati NBC waliwezesha kuendesha mafunzo ya wajasiliamali wapatao 150 kwa vikundi mbalimbali vya wanawake kutoka Kata ya Mjawa,Mahege,Salale,Mwambao na Mlanzi.Mafunzo haya yalitolewa kwa kushirikiana na TanTrade pamoja na SIDO.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA TEHAMA NA UHUSIANO KIBITI .
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.