19 Nov, 2023
Kamati ya siasa mkoa wa Pwani ikiongozwa na Mwenyekiti wake Bw. Mwinshehe Mlao imetembelea Halmashauri ya wilaya ya Kibiti kuangalia jinsi ilani ya chama cha mapinduzi inavyotekelezwa katika halmashauri hii kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo. Mwenyekiti huyo ameongozana na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Katibu wa CCM Mkoa wa Pwani, Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Pwani na Muwakilishi wa jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Pwani.
Kamati hiyo imetembelea miradi miwili ambayo ni Hospitali ya wilaya ya kibiti iliyopo kata ya Mtawanya na Shule ya Msingi Itonga iliyopo kata ya Bungu, hii ni shule mpya kabisa ambayo imekamilika kila kitu ipo tayari kwa matumizi, hivyo inatarajiwa kuanza kufanya kazi Januari, 2024.
Katika majumuisho ya ziara hiyo Bw. Mlao amesema “nimeridhishwa sana na utekelezaji wa ilani ya chama kwa kujenga majengo mazuri, hata hivyo majengo mazuri yaendane na utoaji wa elimu bora”.
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Pwani Bw. Abubakar Kunenge akaongeza “Kama kuna mtu ana mashaka na mambo yaliyofanywa na serikali ya Awamu ya sita basi aje kutembelea Mkoa wa Pwani.”
Sambamba na hayo kamati hiyo pia ilipata nafasi ya kufika kwenye shule mpya ya sekondari inayojengwa kwa nguvu za wananchi ambapo imewapongeza wananchi kwa kujitoa kwao kwa hali na mali ikiwemo kutoa ardhi ambayo shule hyo imejengwa. Bw. Mlao aliwaomba wananchi wawatumie mualiko kamati ya siasa mkoa ili waje rasmi kuitembelea shule hiyo.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.