Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wa Wilaya ya Kibiti kuishi kwa kudumisha amani na utulivu huku akiwasisitiza kufanya kazi kwa bidii Kwa ajili ya kujipatia maendeleo.
" Ili muweze kufanya maendeleo, dumisheni Amani na Utulivu wa Wilaya" Alisema Rais Samia
Amesema hayo baada ya kuwasili katika kituo cha mabasi Kibiti akielekea wilayani Mkuranga kuzindua kiwanda cha kutengeneza vioo vya kutengenezea vyombo vya majumbani (glass ) akitokea mikoa ya Mtwara na Lindi ikiwa ni ziara zake za kawaida nchini na kuahidi kurudi kibiti maalumu kwa ajili ya kuzungumza na wananchi.
Akijibu maombi ya Mbunge wa Jimbo la Kibiti Mhe. Rais Samia amesema, mradi wa barabara ya Lami kutoka Bungu hadi nyamisati, ameuchukua na ataangalia kadri itakavyowezekana kulingana na bajeti.
Kuhusu mradi wa ghala pia ameuchukua huku akisisitiza kuwa kuna wakati inabidi Wilaya kama Wilaya kutafuta fedha kwa namna yeyote ikibidi hata kukopa kuhakikisha miradi inatekelezeka na siyo kusubiri mpaka Serikali itafute fedha.
Vilevile kwa upande wa zoezi la ugawaji wa vitalu vitalu linaloendelea kutekelezwa Wilaya ya Kibiti Rais Samia amesema wanaopewa vitalu hivyo wawe ni wafugaji wanaojulikana siyo kwa mtu yeyote anaehitaji.
" Katika zoezi la ugawaji wa vitalu hakikisheni mnaowagawia wawe wafugaji mnaowajua ( wanaotambulika Wilayani) na siyo tu kwamba watu wanataka vitalu" Alisema Dkt. Samia.
Hata hivyo, Mbunge wa Jimbo la kibiti Mhe. Twaha Mpembenwe akitoa salamu za Jimbo la Kibiti, amempongeza Rais Samia kwa kutoa fedha nyingi za miradi ya maendeleo na kutekeleza miradi mbalimbali wilayani kibiti.
Awali maombi ya Mhe. Mpembenwe yalihusu ujenzi barabara ya lami kutoka Bungu mpka Nyamisati, kupatikana kwa banio kwa ajili ya kilimo cha mpunga pamoja na mradi wa Ghala la mazao.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.