Halmashauri ya wilaya ya kibiti imewasilisha rasimu ya mpango wa bajeti ya Halmashauri katika kikao cha Baraza la wafanyakazi cha mwaka wa fedha 2023/24 na kujadiliwa na wajumbe ambao ni wafanyakazi wa Halmashauri hiyo
Kikao hicho ambacho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri, Afisa Utumishi Sudi Kassim amewashukuru wafanyakazi (wajumbe) wote waliohudhuria kwa namna walivyokuwa makini kufuatilia kuchangia na kutoa maoni ambayo idara ya Utumishi imeyabeba na kuahidi kuyafanyia kazi mapungufu yote na maboresho yaliyobainishwa.
Katika kikao hicho Afisa Utumishi Sudi ambaye ndiye alikuwa Katibu msaidizi amesema kikao cha Baraza la wafanyakazi kipo kihalali na kazi yake kubwa ni kuhakikisha na kuangalia stahiki zote za wafanyakazi, ikiwa ni pamoja na masuala ya likizo,motisha n.k.
Aidha Afisa Maendeleo wa Wilaya Hamis Mnubi ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Baraza hilo amewapongeza na kuwashukuru wafanyakazi kwa kushiriki na kuchangia vizuri ajenda zilizokuwa zikijadiliwa hususani katika michango ya maboresho ya bajeti ya fedha 2023/24.
Vilevile Mwenyekiti Mnubi amesisitiza kuwa mapendekezo,ushauri,maboresho na maoni yaliyotolewa idara husika zimeyabeba na zitayafanyia kazi kwa kuzingatia maslahi ya wafanyakazi na Halmashauri kwa ujumla .
Awali katika majadiliano wafanyakazi wamepitisha ajenda zote zilizokuwa zikijadiliwa ikiwa ni pamoja na kutoa maoni, ya Nini kifanyie au kuboreshwa ili kuweza kusonga mbele. Na Katibu wa chama cha Walimu Wilaya ya Kibiti Crecencia Tingwa amewasisitiza wakuu wa idara kuanza kujiandaa mapema kupanga watumishi hodari sambamba na posho zao kwa kuteua majina kwa kufuata vigezo ikiwa ni maandalizi ya sikukuu ya wafanyakazi duniani (Mei Mosi) ambayo huadhimishwa kila ifikapo 1/5 kila mwaka.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.