Ikiwa ni msimu wa 6 Mfululizo wa tamasha la nifuate SAMAKIBA linalochangisha na kusaidia jamii, leo wamekuja na NIFUATE UPENDO WA ZAMBARAU, IMBA, CHEZA NA MTOTO NJITI kupitia mchezo wa mpira wa miguu uliochezwa katika uwanja wa Azam complex kuanzia majira ya saa 11 jioni .
Kupitia tamasha no hilo Hospitali ya wilaya ya Kibiti imepokea msaada vifaa tiba vyenye thamani ya sh 70,000,000 kutoka kwa wadau mbalimbali wa maendeleo ya samakiba na Doris mollel kwa ajili ya kuchangia na kusaidia watoto ambao wamezaliwa kabla ya muda (NJITI).
Akikabidhi vifaa hivyo Dorris Mollel kutoka Dorris foundation amesema Vifaa tiba vilivyotolewa ni Vitanda vya watoto wachanga 10, Mashine ya kuzalisha hewa ya oxygen 3, Mashine ya umeme ya kuvuta uchafu 1, Mashine ya mguu ya kuvuta uchafu 4, Mipira ya kuvuta / kupitisha uchafu unaovutwa boksi 10, Mabegi ya shule 25 , Vifaa vya kujifungulia 12 , vipima uzito kwa watoto wachanga 2 na ambu bag 10.
"Baby cot 10, oxygen conc. 3, weigh scale 2, pedal suction 4, electrical suction 1, ambu bag 10, suction tube 10 box, delivary kit 12, school bag 25". Kwa majina ya kilaalam. Kiivyo
Vilevile Bi Dorris Alisema vifaa hivyo vilivyokabidhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kibiti, ndivyo vitakabidhiwa pia katika Hospitali ya Wilaya ya Buhingwe mkoani Kigoma.
Mara baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kibiti Denis Kitali ameishukuru Taasisi ya SAMAKIBA kwa kushawishi na kuwezesha upatikanaji wa vifaa tiba Wilaya ya Kibiti, kwani kutokana na uhaba uliokuwepo, vinakwenda kuwa msaada mkubwa wa kutatua changamoto ya watoto waliozaliwa kabla ya wakati (NJITI).
Akipokea vifaa hivyo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Dkt. Elizabeth Oming'o alisema, amefarijika sana kupata msaada huo kwani utaokoa maisha ya vizazi vilivyokuwa vinapotea hususani watoto wanaozaliwa kabla ya muda na wenye uzito mdogo wilayani humo.
Hata hivyo Taasisi ya SAMAKIBA ambao ni Mbwana Sammata na Ally Kiiba kwa nyakati tofauti waliwashukuru wananchi kuhudhuria mechi changizo la vifaa tiba, huku waliwashukuru wadau wote waliojitokeza kwa hali na mali kuhakikisha vifaa vinapatikana kuweza kuisaidia jamii na Serikali kwa ujumla.
Aidha, Rais Mstaafu wa awamu ya nne na mgeni rasmi wa tukio hilo Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amewashukuru na kuwapongeza SAMAKIBA kwa kuwa chachu ya kuchangia vifaa tiba jambo ambalo ni jema sana katika jamii hasa katika vizazi vya sasa.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.