Idara ya Maendeleo ya jamii jinsia Wazee na watoto Wilaya ya Kibiti kwa kushirikiana na wadau mbalimbali washeria,wamefanya uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsi kwa wanawake na watoto duniani Katika Kata ya Bungu B, ambayo huadhimishwa Kila mwaka kuanzia novemba 25 mpaka Disemba 10 ulimwenguni.
Maadhimisho hayo ambayo mwaka huu kauli mbiu ya Kitaifa ni KILA UHAI UNA THAMANI, TOKOMEZA MAUAJI NA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO huazimishwa kwa lengo la kufanya kumbukuzi ya kuwaenzi akina dada wa Mirabal, wanaharakati watatu wa kisiasa kutoka Jamhuri ya Dominika ambao waliuawa kikatili mwaka 1960.
Lengo la Umoja wa Mataifa kupitisha kuadhimishwa kwa siku ya ukatili Duniani ni Kuongeza uelewa wa umma juu ya suala hilo kila mwaka ifikano 25 Novemba na kuhitimishwa Disemba 10 ambapo ulimwengu huadhimisha siku ya haki za binadamu ikiwa ni nafasi nzuri ya kuweza kupaza sauti na kusikika ulimwengu mzima.
Akizungumza kwa niaba ya mgeni rasmi Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Mhe. Ramadhani Mpendu, Mwenyekiti wa kitongoji cha Kibaoni Bungu B Ismaii Mikoi amesema ni wajibu wa Kila mtoto kutoa taarifa anapofanyiwa ukatili wa aina yeyote ile.
Hata hivyo Mikoi amewasihi watoto kuacha tabia ya uoga akisisitiza kutoa taarifa ni muhumu kuanzia nyumbani mpaka ngazi ya juu ili wahusika wachukuliwe hatua stahiki za kisheria .
“ watoto ni viongozi wa baadae fungukeni kutoa taarifa mnapona viashiria au mnapifanyiwa ukatili, tunahitaji kuwa na kizazi chenye Afya Bora”alisema Mikoi.
Aidha amewataka watoto kuwa na tabia ya kutembea kwa makundi hususani katika muda wa kwenda shule, huku akisisitiza kuepuka kutembea mmoja mmoja kwani kumekuwa na matukio ya watoto kupotea, kufanyiwa vitendo viovu na kuuawa kikatili.
Vilevile amewaambia watoto wanapoona mtu anawafatilia na hawamfaahamu wakimbie kutoa taarifa wasikubali kufuatana nao au kuwasikiliza watu wa aina hiyo, lolote na wakiona hawezi kukimbia wapige kelele watu wawasaidie.
Pia amesema hata kama ni mtu mnamfahamu anakuwa na dalili hizo usiogope, toa taarifa au mpigie kelele anapojaribu kukufanyia ukatili.
Aidha amesema kutokana na elimu iliyotolewa kuhusu ukatili wa kijinsia ni imani yake watoto wameelewa na anatarajia kupokea taarifa kwa kila atakayefanyiwa ukatili wa kijinsia muda wowote ule .
Uzinduzi wa ukatili wa kijinsia uliambatana na burdani kwa michezo mbalimbali kama vile maigizo,kwaya ,mpira wa miguu,kukimbia kwa gunia na kukimbiza jogoo.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.