SIKU YA PILI
Hatimaye muafaka wa jinsi gani Shirika la Wetland international litashirikikiana na jamii kulinda na kuhifadhi misitu ya mikoko delta ya rufiji katika Wilaya ya kibiti umepatika kwa kupitisha maadhimio mbalimbali yatakayoanza kutekelezwa rasmi mwakani baada ya wadau kutoa maoni na kukubaliana.
Hayo yamebainishwa katika majadiliano yaliyodunu kwa siku 2 katika ukumbi mikutano wa Halmashauri Wilaya ya Kibiti ambapo wadau wamekubaliana utekekezaji wa kuhifadhi mikoko kuanza sasa sambambakuzitaka mamlaka husika kupitia upya sheria za uhifadhi wa mikoko na delta na kuunda sheria ndogo, kwa kuweka kipaumbele cha uhifadhi shirikishi kwa kipindi cha miaka 30 huku wakisisitiza viongozi wote wa delta kusimamia majukumu yao ipasavyo. Pia wameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti kutoa wataalamu wao kutekeleza majukumu yaliyoainishwa ambayo wakisaidiana na Taasisi ya wetland ili jamii itambue faida zitokanazo na mikoko.
Ili kufika malengo ndani na nje ya delta Kwa miaka 30 ijayo,wanarsha wamekubaliana kutoa Elimu Kwa jamii kujua faida ya mikoko Kwa njia ya maigizo,vipeperushi na mikutano ya hadhara,kubaini na kuweka mikakati ya kulinda na kuhifadhi maeneo ambayo hayajaathirika,kubaini na kurejesha uoto wa asili kwa maeneo yaliyoathirika,kuanzisha njia mbadala za kiuchumi kama vile kilimo,ufugaji wa nyuki,utalii na uvuvi wa kisasa ikiwa ni pamoja na kuanzisha mfuko maalum kwa lengo la kulinda na kuendeleza uhifadhi wa mikoko na kuziwezesha jamii zinazoishi delta.
Vilevile katika mjadala huo wadau wamesema kinachochangia kuharibu uoto wa asili kwa maeneo ya delta ni pamoja na kufanyika kwa shughuli za uvunaji wa mbao kwa kukata mikoko,uvamizi wa idadi kubwa ya wafugaji,kilimo cha mpunga kisicho rafiki,utupaji taka na uchomaji wa moto ndani ya misitu.Wakati huo huo wakakubaliana kufanyika marekebisho Kwenye Sheria kubwa na ndogo za kudhibiti aina zote za uvuvi haramu kwa kufanya doria,pia kufanyika marekebisho kwenye Miradi inayotekekezwa na itakayotekelezwa pamoja na kuiwezesha kamati ya maliasili na TFS kushirikiana katika utekekezaji.
Hata hivyo wanawarsha wamesema Ili kuhifadhi mikoko Kuna Kila sababu ya uhitaji wa kuimarisha usimamizi wa mikoko,kuimarisha huduma za kijamii maeneo ya delta,kutoa elimu ya uvuvi endelevu, ufugaji endelevu na kilimo endelevu chenye tija,pia kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo na kutunga sera itakayowezesha kufanya biashara ya hewa ukaa.
Aidha eneo la Pwani ya Rufiji linatarajiwa kunufaika na asilimia 30 ya mapato yatokanoyo na shughuli za uhifadhi wa mikoko Kwa ujumla hivyo wadau hao wameiomba Serikali kuzuia na kuondoa mifugo maeneo ya delta, kusimamia uendeshaji wa misitu na uhifadhi wa mikoko,kuboresha miundombinu ya barabara ,mitaro na umeme ikiwa ni pamoja na kutambua thamani ya na (mtu binafsi) vinavyohusika na uhifadhi wa mikoko.
Wetland international ni shirika/taasisi isiyo ya kiserikali inayojishughulisha na kazi ya kulinda na kuhifadhi ukanda wa ya delta ya Rufiji Tanzania katika maeneo oevu hususani katika Wilaya ya kibiti ambapo kati ya aina 7 ya mikoko inayopatikana bara la Afrika 6 hupatikana kibiti pekee.ukiacha Tanzania Wetland international hufanya kazi na nchi za Uganda,Sudan kusini, Ethiopia na Senegal.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.