Kuelekea kilele cha siku ya Wanawake duniani, Wanawake wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti wamewatembelea watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu waliopo katika kituo cha Mataqwa ya Waislam katika Kata ya Bungu ili kutoa Faraja na kuwapa zawadi mbalimbali.
Zawadi zilizoolewa ni Mchele Kg 80, Unga Kg 50, Sukari Kg 25, Maharagwe Kg 30, Mafuta ya kupikia Lita 10, Sabuni ya unga Mfuko 1, Sabuni ya mche Boksi 1, Mafuta ya kupaka Katoni 3, Dawa za meno Boksi 3, Juisi Katoni 20, Taulo za kike Katoni 1 pamoja na nguo.
Hiyo yote ni michango ya Wanawake watumishi wa Halmashauri, Wafanyabiashara, Wakulima pamoja na Taasisi mbalimbali.
Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Wilayani Kibiti yanafanyika leo tarehe 8 Machi, 2024 katika Uwanja wa Samora.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.