Hatimaye mgogoro wa mipaka kati ya mwekezaji wa kilimo cha mpunga Bw. Khamisi Kambanga katika Kijiji cha mtunda A na Kijiji cha Muyuyu Wilayani Kibiti Mkoani Pwani umepata suluhu baada ya kupata maridhiano ya wananchi katika vijiji hivyo.
Akizungumza na Wananchi wa Vjiji hivyo, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Meja Edward Gowele amemtaka mwekezaji huyo kuendelea na kazi zake katika Kijiji cha Mtunda A kwani yupo ndani ya mipaka sahihi.
Vile vile amemrejesha kazini Mwenyekiti wa Kijiji cha Muyuyu ndg Hassan Mtendwe ambaye aliondolewa madarakani na wananchi wa Kijiji hicho pasipo kufuata taratibu za kisheria huku wakidai kuwa hawana Imani na kiongozi huyo.
Awali Meja Gowele aliiagiza Idara ya Ardhi Wilayani humo Pamoja na kamati tendaji ya vijiji hivyo viwili kufanya tafsiri ya mipaka ili kubaini uhalali wa mpaka uliokuwa ukileta mgogoro na kusababisha wananchi wa Vijiji hivyo viwili kulumbana.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.