Taasisi ya Elimu Tanzania(TET) imeanza kuendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo Walimu wa Sekondari Wilaya ya kibiti juu ya mfumo mpya wa ufundishaji na ujifunzaji Compitence based curriculum kuanzia TAREHE 16 na kumalizika TAREHE 27 mwezi Januari
Akizungumza katika ukumbi wa mikutano wa shule ya sekondari Kibiti Mkurugenzi kutoka Taasisi ya Elimu Daktari Fika Mwakabungu amesema, changamoto kubwa inayosababisha watoto kufeli ni pamoja na walimu kushindwa kuunda mbinu za ujifunzaji na ufundishaji ambazo zitakazosaidia mwanamfunzi kuwa na uwezo mkubwa wa kufikiri .
Katika utangulizi Mkurugenzi Mendaji wa halmashauri ya kibiti Mohamed Mavura amesema hali ya Taaluma Wilaya ya kibiti kwa Miaka mitatu mfululizo hairidhidhi ni mbaya kwani ufaulu wa kidato cha pili umeshuka kutoka Asilimia 85 – 66 Mpaka kufika Mwaka huu.
Vilevile Mavura amesema mafunzo Hayo yanafanyika Kwa makusudi ya kuleta mapinduzi ya elimu ikiwa ni tumaini lake kuwa mafunzo hayo yatasaidia kuwajengea Walimu uwezo mzuri wa ufundishaji na ujifunzaji wa kupitia mfumo mpya wa mitaala yaani Compitence based approach utakaokwenda kuinua kiwango Cha ufaulu huku akisisitiza kufumua waratibu wa Elimu wote na walimu wakuu kwani wengi wao hawafanyi kazi ipasavyo.
Aidha katika uzinduzi wa mafunzo hayo, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Meja Edward Gowele ameagiza kufanyika Kwa Kikao Cha Wazazi Ili kujadili suala zima la elimu kwani Wazazi ni chanzo Cha watoto kushindwa kwenda shule ipasavyo. Pia Mhe. Gowele amesema kuwa ni kutoitendea haki Serikali katika jitihada za kutomeza zero ukizingatia Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ametoa fedha nyingi kuhakikisha shule zinajengwa katika maeneo ya karibu na jamii huku akiagiza kuwa ifikapo tarehe 29 January anahitaji kupata taarifa ya watoto wote wameripoti shuleni.
Pia amemuagiza mkurugenzi Mtendaji Mohamed Mavura kutowafumbia macho walimu wazembe sambamba na walimu ambao ni watomvu wa nidhamu ikiwa ni pamoja na kujihusisha kimapenzi na Wanafunzi.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.