Tume ya Taifa ya uchanguzi (NEC ) imeanza zoezi la uhakiki wa maeneo ya Kiutawala Wilayani Kibiti ikiwa ni mkakati Maalum wa maandalizi kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Akiongoza kikao hicho katika ukumbi mdogo wa mikutano wa Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji, Afisa wa Tume ya uchaguzi Bi Rehema Wambura amesema lengo la kikao hicho ni kufanya ukaguzi wa awali wa maeneo ya Kiutawala pamoja na kuchukua changamoto ambazo zinaweza kujitokeza katika zoezi la Uchaguzi na kuzitafutia ufumbuzi mapema.
Mara baada ya Kupokea ugeni huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Mohamed Mavura amewataka Watendaji wa Kata wote, kutekeleza majukumu yao kwa umakini na kutambua mipaka ya maeneo yao ya kiutawala.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji, amewasisitiza Maafisa wa Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) kuchukua changamoto zote zilizoletwa na Watendaji wa Kata na kuzifikisha mahali husika kwa kuzisemea kiuhalisia kulingana na jiografia ya Mazingira ya wilaya ya Kibiti hususani maeneo ya Visiwani (Delta).
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.