KIKAO CHA VYAMA VYA SIASA SHIRIKI KATIKA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI KATIKA KATA YA MAHEGE TAREHE 24/06/2023.
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kibiti Ndugu Hemed Magaro amewakilishwa na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Jimbo la Kibiti Ndugu Theonest Kibuga na Afisa Uchaguzi katika Jimbo la Kibiti Ndugu Sudi Khassim wameendesha kikao na Viongozi wa vyama vya siasa shiriki kwa lengo la kupeana Elimu na kukumbushana hatua mbalimbali za Uchaguzi mdogo wa Diwani katika kata ya Mahege.
Wenyeviti na Makatibu wa Vyama vya Siasa walioshiriki katika kikao hicho ni kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Chama cha ACT Wazalendo na Civic United Front (CUF).
Aidha katika Kikao hicho Afisa Uchaguzi katika Jimbo la Kibiti Ndugu Sudi Khassim, aliwapitisha Viongozi wa vyama katika ratiba nzima ya zoezi la Uchaguzi, Mada kuhusu uteuzi wa wagombea pia ilitolewa ikibainisha taratibu za uchukuaji na urejeshwaji wa fomu za Uteuzi, mambo yanayotakiwa kufanywa na yasiyotakiwa kufanywa na aliwakumbusha uzingatiaji wa sheria, kanuni, taratibu na maadili katika Uchaguzi.
Mwisho, Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Jimbo la Kibiti Ndugu Theonest Kibuga aliwapatia Viongozi wa vyama vya siasa vitabu vya Maelekezo ya vyama vya siasa na Wagombea na kuwaasa kusoma kwa umakini vitabu hivyo huku akiwakumbusha uzingatiaji wa Amani, Staha na Utulivu wakati wa Mchakato wa Uchaguzi Mdogo wa Udiwani katika Kata ya Mahege.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.