Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kibiti Mohamed Mavura akiwa ameambatana na wataalam mbalimbali wa Halmashauri, wamekagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya Wilaya kwa vyanzo mbalimbali vya mapato ili kujionea hatua zilizofikiwa.
Wakiwa katika kata ya Dimani wamekagua mradi wa ujenzi wa zahanati ya Nyambangala wenye thamani ya sh 72,000,000 kwa fedha za mapato ya ndani na ujenzi upo katika hatua ya ukamilishwaji.
Vilevile wamekagua mradi wa zahanati ya Kitembo katika kata ya Kibiti ambao upo katika hatua ya umaliziaji. Ujenzi huo wenye thamani ya sh 68,849,000/= ulioanza kwa nguvu za wananchi hadi hatua ya boma, na baadae kupokea kiasi cha Tsh. 50,000,000/= kutoka Serikali kuu kwa ajili ya ukamilishwaji, hata hivyo Halmashauri iliongeza kiasi cha Tsh 18,849,000/= kwa ajili ya umaliziaji.
Mbali na miradi hiyo wamekagua ujenzi wa Jengo la kuhifadhia maiti, Jengo la upasuaji, wodi la wanaume na wanawake katika Hospitali ya wilaya wenye thamani ya sh 800,000,000 kwa fedha za Serikali kuu ambapo ujenzi upo hatua ya umaliziaji.
Pia wamekagua mradi wa ujenzi wa nyumba 4 za walimu katika shule ya msingi Pagae iliyopo katika kata ya Bungu, unaofadhiliwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TEA). Mradi huo unathamani ya Tsh. 100,000,000 na upo katika hatua ya upandishaji kuta.
Vilevile katika kata ya Mjawa wamekagua Shule ya sekondari Jaribu mpakani Mradi unaotekelezwa kwa fedha za SEQUIP na kituo cha Afya Mjawa mradi unaotekelezwa kwa fedha za Tozo za Miamala ya simu.
Aidha kwa nyakati tofauti Mkurugenzi amemuagiza Mkandarasi wa Wilaya Pamoja na Idara ya manunuzi kuhakikisha kuwa vifaa vyote vinapatikana maeneo ya ujenzi kwa wakati pia mafundi wawepo maeneo ya kazi na wahakikishe kuwa kazi inafanyika ya uhakika ili kuweza kukamilisha kwa wakati.
Mbalina hayo Bwana Mavura ameagiza kusitishwa kwa mkataba wa Mkandarasi wa kituo cha afya Mjawa na shule ya sekondari jaribu mpakani na kutafuta fundi makini anayeweza kuendana na muda Pamoja na viwango bora vya kazi.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.