Tarehe 9/3/2023
Ujenzi wa vyumba 5 vya madarasa na ofisi ya walimu Katika shule ya msingi Kiasi wenye thamani ya sh 110 ulioanza mwaka 2022 umekamilika na madarasa yameanza kutumika.
Timu ya usimamizi wa majengo ya shule hiyo ambayo ipo Katika Kata ya msala, imewasili na kukagua Ujenzi uliokuwa ukiendelea kwa lengo la kujionea hali halisi na kujiridhisha.
“ Tumekuja kujionea na kuhakikisha, hali halisi ya ujenzi ulipofikia, tumefarijika madarasa yamekamilika”Alisema Mlenduka.
Awali shule hiyo ilitengewa fedha kwa ajili ya ukarabati, lakini kutokana na uchakavu wa shule hiyo, kamati iliona ni vema kuvunjwa na juanza kujenga upya.
Vilevile Mlenduka amefafanua kuwa, vyanzo vya fedha vya Ujenzi huo wenye jumla ya sh 110,000,000, sh 100,000,000 ni fedha za serikali Kuu kupitia mradi wa EP4R na 10,000,000 ni fedha za Mapato ya ndani ya wilaya.
Aidha mtaalamu wa majengo Mhandisi msaidizi wa Wilaya Juma Kubadesha mara baada ya kuwasili shuleni hapo alikagua majengo na kuthibitisha kuwa ujenzi umekamilika kwa 100% Kubadesha amesisitiza uongozi wa shule na wanafunzi kwa ujumla kuyatunza vizuri majengo na samani zilizopo ili viweze kudumu kwa muda mrefu.
Mbali na ukaguzi wa majengo hayo, Afisa Elimu akiongozana na wasaidizi wake wamefanya ukaguzi na ufuatiliaji juu ya utekelezaji wa KPI (Key Performance Indicators) katika shule hiyo, ambapo wamejionea shule hiyo inatoa huduma ya chakula cha mchana, mkazo wa ufundishaji somo la kingereza kwa darasa la tatu upo vizuri, na katika suala la KKK darasa la 4 wote wanajua vizuri Kusoma, Kuandika na Kuhesabu isipo kuwa wanafunzi wa chache wa darasa la pili na la tatu bado wanapata shida kusoma herufi mbwambatano. Hata hivyo maandalizi ya madarasa ya mitihani yanakwenda vizuri hivyo tunategemea ufaulu utaongezeka.
Katika ziara hiyo iliyoongozwa na Afisa Elimu divisheni ya elimu msingi (DEO- P) aliambatana na Maafisa Taaluma, Afisa Elimu Takwimu- msingi, Afisa msaidizi Mipango, SNEO na Mhandisi wa majengo.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.