30.04.2024
Shirika la kimataifa la kuhudumia watoto ulimwenguni (UNICEF) linaloshughulikia masuala ya kijamii limetembelea kambi kuu ya kitumbini Wilayani Kibiti kwa lengo la kujionea hali halisi na mazingira ambamo waathirika wa mafuriko wanaishi tangu walipohamia rasmi baada ya mvua kubwa ninazonyesha nchini kusababisha mafuriko yaliyopelekea wananchi kukosa makazi.
Ziara hiyo iliongozwa na Mkuu wa Idara ya Mipango Uratibu na Ufuatiliaji kutoka UNICEF Bi.Christine Hofer ambaye aliambatana na Bw. Stanislaus Kamwaga Mhandisi wa Idara ya maji na Mazingira - UNICEF pamoja na Bi. Penina Sangiwa kutoka Idara ya Elimu - UNICEF.
Mara baada ya wawakilishi hao kuwasili Kambini na kujionea hali halisi wameahidi kuwa katika kipindi hiki, UNICEF itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha hali ya Mazingira ya waathirika hao inaimarika.
Mbali na kutembelea kambi hiyo pia wametoa msaada wa matenki 12 yenye ujazo wa lita 5000, ndoo 907 za lita 20 zenye koki, sabuni za maji, mahema makubwa 4, mahema madogo 5, na vifaa binafsi vya kujikinga kama vile magwata (gumboots), gloves, maski, eproni, chrorine, jerrycanes n.k
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.