17.4. 2024
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Ndg. Mary Chatanda amewaasa wakazi wa maeneo ya delta katika Wilaya za kibiti na Rufiji kuacha kutumia usafiri wa mitumbwi katika kipindi hiki kwani ni hatari kwa Usalama wa maisha yao kutokana na wingi na kasi ya maji yanayopita katika mto Rufiji.
"Angalizo Ndugu zangu katika kipindi hiki tuelimishane, maji ni makali mno, yana kasi kubwa kiasi kwamba huweza kupindua mtumbwi na kusababisha maafa, sikilizeni wataalamu wanawaelekeza nini msipuuze" Alisema
Bi Chatanda amesema hayo leo wakati akitoa salam za pole kwa waathirika wa Mafuriko Wilaya ya Kibiti wakiwa katika ukumbi wa shule ya wavulana Kibiti ambapo ni kituo kikuu cha mapokezi ya misaada ya janga hilo.
Akiwa katika viunga hivyo ndg Chatanda amemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Pwani vifaa mbalimbali vilivyoandaliwa na UWT ambapo amebainisha Misaada iliyotolewa ni shuka 470, vyandarua 400, vijora 500, unga wa sembe viroba 76, maharagwe kg 100, sukari kg 150 na ndoo kubwa za plastic 380.
Vifaa vingine vilivyotolewa ni mabeseni 400, sahani 442, vikombe 492,magodoro 47, nguo za watoto belo 1, nguo za watoto wa kike belo 1, nguo mchanganyiko begi 3, mabegi ya shule 35, pampas pisi 10, viatu mchanganyiko kiroba 1 na tambi mifuko 10.
Licha ya msaada huo pia wamekabidhi sabuni za mche boksi 10, sabuni za unga viroba 2, masufuria makubwa 5, MADAFTARI 500, mafuta ya kupikia ndogo 3, mafuta ya kupikia korie boksi 5, unga wa ngano kg 25 viroba 3, blanket belo 3 na mikeka 3.
Hata hivyo mara baada ya kupokea msaada huo Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe.Abubakar Kunenge amewashukuru UWT TAIFA kwa msaada mkubwa walioutoa na kuwahakikishia kuwa msaada huo utawafikia walengwa kama iliyokusudiwa.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amepokea magodoro 200 na vyandarua 200 kutoka Kampuni ya save the children, na misaada mingine aliyopokea ni maharagwe kg 100, mchele kg 100, unga kg 500 mafuta ya kupikia lita 100 na sukari kg 100 kutoka Kampuni CRCEB.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Joseph Kolombo alipokea magodoro 300, mafuta ya kupikia lita 250, sukari kg 250, unga kg 250 na mchele kg 250 kutoka Kampuni ya Superdoll.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.