WAKEMEA SUALA LA MASHOGA NCHINI.
19/3/2023.
Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) umemwomba Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, kuweka sheria kali kuhusu tabia ya ushoga ambayo imekuwa ni changamoto ulimwenguni na kuwa janga katika maeneo mbalimbali hata Kwa Tanzania.
“Mhe. Rais, Wanawake tunashauri iundwe sheria kali ya kukemea ushoga nchini, na wahusika wa tabia hizo wakipatikana ikiwezekana wahasiwe” Alisema Chatanda
Hayo yamejiri katika hafla ya kuadhimisha miaka 2 ya Rais Samia madarakani tangu alipochaguliwa machi 19/2021 baada ya aliyekuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano Mhe. John Pombe Magufuli kufariki dunia machi 17 mwaka 2021.
Akihutubia wananchi waliohudhuria katika uwanja wa uhuru jijini dar es salaam ambapo sherehe hiyo ilifanyika Mwenyekiti wa UWT Taifa Bi. Mary Chatanda amesema, lengo la UWT kufanya sherehe hiyo ni kumpongeza Rais kwa kutimiza miaka miwili madarakani akiwa amepiga hatua kubwa kwa kuleta maendeleo hususani kwa wanawake kiuchumi na kijamii.
“Tupo hapa kumpongeza Rais, kwani tumeshuhudia kazi nzuri za maendeleo alizozifanya ndani ya miaka 2” Alisema Chatanda.
Akimpongeza Mhe.Rais Samia, Mwenyekiti Chatanda alisema, tangu Rais Samia aingie madarakani, ameonyesha ushupavu kwani ametoa mchango mkubwa kulinda na kusimamia sheria ipasavyo huku akiahidi kwa niaba ya wanawake wote kuwa, wanawake kwa umoja na mshikamano wao ajenda yao ni moja 2025 kuhakikisha anarudi madarakani.
“mkusanyiko wa Wanawake waliojitokeza hapa leo, ni ishara tosha kuwa tuko pamoja,tutashirikiana bega kwa bega” alisema chatanda.
Licha ya pongezi hizo, UWT imetoa zawadi ya TUZO na picha kwa MHE Rais ikiwa ni ishara ya kumuunga mkono na kumtia moyo Kwa namna alivyoweza kuwa mwanamke wa mfano.
Aidha Katibu wa UWT Taifa Zainabu Shomari katika maadhimisho ya utendaji wa Rais amesema UWT imetambua na kuona juhudi za maendeleo katika kada mbalimbali nchini zilizofanywa na Rais ndiyo maana wameamua kumpongeza.
Ndani ya miaka miwili Mhe. Rais ameweza kusimamia kikamilifu hali ya kisiasa nchini, utulivu ndani ya nchi, uimarishaji wa kada ya afya ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Hospitali za Wilaya, vituo vya afya, ujenzi wa jengo la wagonjwa wa dharula na zahanati sambamba na utoaji wa vifaa tiba.
Vilevile Shomari aliendelea kusema mbali na hayo pia Rais ametoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa shule nchini, miundombinu ya maji, barabara, reli na umeme unaendelea kuimarishwa, bila kusahau alivyowajali wanafunzi wa vyuo vikuu kwa kuwaongezea mkopo kutoka 8000 - 10000 kwa siku.
Sherehe hiyo iliyoratibiwa na chama umoja wa Wanawake Tanzania imehudhiriwa na wanawake wote wa UWT Tanzania na wananchi mbalimbali wanawake, kwa wanaume.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.