Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Meja Edward Gowele na mgeni rasmi amefunga mafunzo ya Jeshi la Akiba kundi la 06/22 katika kituo cha Mtawanya yaliyoanza mwezi Julai na kukamilika Novemba 2022.
Katika ghafla hiyo Meja Gowele amewapongeza vijana 81 waliohitimu mafunzo hayo na kuwataka kufanya kazi Kwa uaminifu na uzalendo na si vinginevyo kama walivyokula kiapo kwani kazi za jeshi zinafanywa Kwa utii na nidhamu kubwa.
Vilevile Gowele ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti kwa namna walivyoshiriki kuhakikisha mafunzo yanakamilika na kulitaka Baraza la Madiwani kutenga bajeti za kusimamia masuala ya ulinzi na usalama
Akijibu maombi ya wahitimu kupita risala na taarifa waliyosoma na kumkabidhi mkuu wa Wilaya ameitaka jamii na Taasisi mbalimbali kujitolea kuchangia gharama za mafunzo hayo kwani jambo la ulinzi na usalama ni la wote katika jamii.
Naye Shabani Mabula, akisoma risala ya utii kwa niaba ya wahitimu wa mafunzo ya wahitimu wa jeshi la Akiba amesema jumla ya vijana 81 wamehitimu mafunzo hayo ambapo 9 ni wanawake na 72 ni wanaume ambao kati yao Bw. Meshark Mabwai aliongoza kwa kuwa na umri mkubwa zaidi (62) kupita wote katika mahafali hayo ambapo alitunukiwa zawadi ya fedha na Mkuu wa Wilaya kama sehemu ya motisha kwa kutokujali umri wake na kuamua kujitolewa kufanya mafunzo kwa uzalendo mkubwa.
Aidha wahitimu hao mbali na kuomba kuchangiwa gharama za mafunzo ikiwa ni pamoja na mavazi na chakula Cha wakufunzi, pia wameomba kupewa kipaumbele cha ajira katika makampuni mbalimbali, Pamoja na kupewa kipaumbele kupata nafasi za jeshi la kujenga Taifa ( JKT) pindi nafasi zinapotolewa
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.