• Malalamiko
    • Wasiliana Nasi
    • Maswali na majibu
    • Barua pepe
KIBITI DISTRICT COUNCIL
KIBITI DISTRICT COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serekali za Mitaa HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBITI

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira
      • Ujenzi na Zima Moto
      • Fedha na Biashara
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo na Umwagiliaji
    • Vitengo
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama na Uhusiano
      • Nyuki
      • Uchaguzi na Utawala Bora
  • Fursa za Uwekezaji
    • Ufugaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Vivutio vya utalii
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Sheria
    • Taarifa
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Taarifa kwa Umma
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Mifumo

WALIMU WA KIBITI WAPIKWA KUFUNDISHA SOMO LA KIINGEREZA. DC KOLOMBO ATARAJIA KUONA UFAULU UKIONGEZEKA.

Posted on: December 17th, 2023

12.12.2023.

Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti imeanza mkakati mpya wa kupandisha ufaulu kwa kuhakikisha wanafunzi wanakuwa na msingi mzuri wa lugha ya kiingereza ambayo imeonekana kuwa changamoto kwa wanafunzi katika kujifunza.

Lugha ya kiingereza ilikuwa inaanza kufundishwa darasa la tatu, sasa itaanza kufundishwa kuanzia darasa la kwanza hatua itakayosaidia watoto kuweza kujieleza na kuwa na msingi mzuri wa lugha hiyo.


Mafunzo hayo yamefanyika katika shule ya Msingi Kitundu Wilayani humo na kufunguliwa rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Kanali Joseph Kolombo.

Halikadhalika mafunzo hayo hayamewezeshwa na  Sofia Amas pamoja na  Albert Kitali wakufunzi kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) ambayo inajihusisha na ukuzaji wa mitaala nchini.

Wakufunzi hao kwa nyakati tofauti walisema lengo la mafunzo ni kuwezesha walimu kufundisha somo la kiingereza kwa ufasaha, ambapo pia mafunzo yatawasaidia kufundisha stadi za kusikiliza, kusoma na kuandika.


"Tuko hapa kuendesha mafunzo ya siku mbili ya somo la kiingereza kwa walimu wanaofundisha darasa la kwanza na la tatu ambapo tumejikita kwenye KKK kwasababu, zitasaidia mtoto kuwa na msingi mzuri atakapoingia darasa la tatu, kama vile kutambua sauti, kuumba maneno n.k” walisema Wakufunzi hao

"Tunaamini baada ya mafunzo haya, walimu wataleta mabadiliko chanya katika ufundishaji na ujifunzaji wa somo la kiingereza kwani ni tegemeo letu kuwa, wanafunzi watapata maarifa na ujuzi wa kuongea kiingereza na kuongeza ufaulu" walisema wakufunzi.


Aidha, Afisa Elimu wa Wilaya ya Kibiti Mwl. Zakayo Mlenduka alisema mafunzo hayo yamefika muda muafaka kwa sababu sera mpya inaelekeza somo la kiingereza kuanza kufundishwa kuanzia darasa la kwanza mpaka la sita tofauti na ilivyokuwa awali kuanza kufundishwa darasa la tatu.

"Tunamshukuru Mkurugenzi Mtendaji Bw.Hemed Magaro kwa kuwezesha mafunzo haya, ambapo fungu limetoka kwenye  mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti ili walimu waweze kupatiwa mafunzo hayo" Alisema Mlenduka.


Akifungua mafunzo hayo Kanali Kolombo kipekee amemshukuru Mkurugenzi Mtendaji Bw. Hemed Magaro na wasaidizi wake kwa kuliona hilo na kulipa kipaumbele, kwani lugha ya kingereza ndiyo lugha kuu ya mawasiliano katika ulimwengu tunaoishi wa Sayansi na Teknolojia.

"Ninamshukuru Mkurugenzi kwa kuliona hili na kutenga fedha kwa ajili ya kuwaandaa walimu hawa kupatiwa mafunzo ya Mtaala mpya wa ufundishaji" Alisema Kolombo.

Hata hivyo aliwataka walimu walioshiriki mafunzo hayo kuitumia fursa hiyo adhimu waliyoipata kuelewa vizuri ili wakaweze kumudu kufundisha somo la kiingereza na kuinua ufaulu ndani ya Wilaya.

"Ni matarajio yangu baada ya mafunzo haya mnakwenda kuwa na mbinu na mikakati mipya ya kuhakikisha watoto wanaweza kumudu somo la kiingereza "Alisema Kolombo.

"Ninajua walimu mnachangamoto nyingi sana, lakini isiwe kikwazo cha kutotimiza wajibu wenu, endeleeni kuchapa kazi Serikali ipo makini nanyi".

Matangazo

  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA MAENEO YA UCHAGUZI HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBITI September 16, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI BODI YA ELIMU April 04, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA February 26, 2024
  • MWALIKO WA WATAZAMAJI February 16, 2024
  • Angalia Vyote

Habari Mpya

  • KANALI KOLOMBO AIPONGEZA MARINE PARKS KUANZISHA MIUNDOMBINU YA KUHIFADHI NA KULINDA MATUMBAWE BAHARINI

    May 10, 2025
  • KIBITI YAPOKEA CHANJO YA MIFUGO.

    May 08, 2025
  • JAJA KUFAIDIKA NA UTALII IKOLOJIA KUPITIA FUKWE .

    May 06, 2025
  • MWENGE WA UHURU WAPOKELEWA WILAYANI KIBITI NA KUTEMBELEA MIRADI 13

    April 08, 2025
  • Angalia Vyote

Video za Shughuri za Ofisi au Kitaifa

More Videos

Kurasa za Haraka

  • Ajira
  • Madiwa wa sasa
  • Barua pepe
  • Wasiliana nasi
  • Malalamiko
  • Maswali na Majibu
  • Fursa za Uwekezaji
  • Maktaba ya Picha
  • Fomu Mbalimbali
  • Facebook: kibitidc

Tovuti zinazoshabiana

  • TANZANIA GOVERNMENT PORTAL
  • COAST REGION WEBSITE
  • TAMISEMI
  • PRESIDENT'S OFFICE,PUBLIC SERVICE MANAGEMENT AND GOOD GOVERNANCE
  • NECTA
  • TOVUTI YA AJIRA
  • IKULU
  • TANZANIA BUREAU OF STATISTIJS
  • Tume ya uchaguzi Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana Nasi

    Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Kibiti

   

    • Sera binafsi
    • Kanusho
    • Maswali na majibu
    • Sitemap
    • Huduma zetu

Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.