31.5.2024
Afisa Elimu Divisheni ya Awali na Msingi Mwl. Zakayo Mlenduka amefungua mafunzo kabilishi kwa walimu wakuu kuhusu mtaala ulioboreshwa mwaka 2023 utakaowaandaa watoto kuhitimu wakiwa na ujuzi.
Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Mwl. Mlenduka ameishukuru Serikali kwa kusikia kilio Cha jamii kwani kwa MTAALA huo ulioboreshwa watoto watahitimu Elimu Msingii wakiwa na ujuzi mbalimbali na masomo ya darasani pia.
Pia amewashukuru wakufunzi na walimu kwa kufika kwenye mafunzo amewaasa kuwa wasikivu ili wakitoka hapo walimu na jamii wakanufaike kwa walichofundishwa.
"Mnategemewa kwa mafunzo haya mnayopewa mkaelimishe jamii kwa kuwashauri watoto kuwa na Uchaguzi bora wa kipi anachotaka kusoma" Alisema.
Naye Mratibu wa mafunzo ya Walimu Wakuu wa shule wa Wilaya ya Kibiti Mwl. Oscar Msalila amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo walimu wakuu kuhusu maboresho ya MTAALA ili wakaweze kuwezesha walimu wao katika shule zao wanazozisimamia.
"Tunawajengea uwezo walimu wakuu ili wakaweze kuwezesha pia walimu wao mbinu za ujifunzaji na ufundishaji pamoja na matumizi ya TEHAMA" Alisema.
Hata hivyo Mkufunzi huyo amesisitiza viongozi wa Kibiti kuhakikisha wanafuatilia utekelezaji wa mafunzo hayo kwani Serikali inatoa fedha nyingi kuhakikisha ufanisi wa ufundishaji na ujifunzaji katika shule zote za msingi nchini.
Aidha mwisho wa mafunzo hayo baadhi ya washiriki wakiwemo Walimu wakuu wa shule ya Mjawa Mwl. Zaina Sengwira na Mwl Rashid Ausi wa Tomoni wamesema mafunzo yamewapatia uelewa mkubwa wenye namna mpya ufundishaji na ujifunzaji na utawasaidia kujenga mahusiano mazuri kati ya walimu wakuu, walimu wengine pamoja na wanafunzi. Pia wamesema Kupitia dhana hiyo wanakwenda kuzalisha wanafunzi walio bora zaidi na wenye kuweza kujikwamua baada ya kuhitimu masomo yao.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.