Wasimamizi wa vituo na wasimamizi wasaidizi wa vituo vya kupigia kura wakiapa mbele ya Msimamizi wa uchaguzi jimbo la kibiti Ndg. Hemed Magaro leo tarehe 17 Machi, 2024 kabla ya kuanza mafunzo kwa wasimamizi hao kwaajili ya uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Mlanzi utakaofanyika tarehe 20 Machi, 2024.
Mara baada ya kula kiapo Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Kibiti alifungua mafunzo hayo yaliyofanyika katika Shule ya Sekondari Mlanzi iliyopo Kata ya Mlanzi Wilayani Kibiti, ambapo wasimamizi waliweza kujifunza ilivyokusudiwa kwa nadharia na vitendo kwa kufuata muongozo wa Tume ya uchaguzi Tanzania.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.