Taasisi ya MAMA ONGEA NA MWANAO imeitembelea Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti na kugawa viatu jozi 200 na hijabu 100 kwa watoto wa shule 2 za Msingi ambazo ni shule ya msingi Mwangia na Kimbendu..
Taasisi hiyo iliyoambatana na wasanii mbalimbali wakiunga mkono kampeni ya Samia nivishe viatu iliyozinduliwa hivi karibuni nchini na Mhe. Rais Samia Suhuhu Hassan wamesema wanatarajia zoezi hilo kuwa endelevu ambapo katika zoezi hilo Kila shule watoto 100 wamepata viatu vipya na Kila shule pia watoto 50 wamepata hijabu.
Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Steve Mengele arimaarufu Steve Nyerere amesema kutokana na hali za uchumi wa watanzania wazazi wengi wanamudu kununua sare za shule na siyo viatu hivyo Kuna Kila sababu ya MAMA ONGEA NA MWANAO kuunga mkono kampeni ya Samia nivalishe viatu na inawezekana kwani kiatu ni safari.
Akizungumzia maadili Steve Nyerere amesema Kuna haja ya kuimarisha siku ya vipindi vya dini shuleni kama ilivyokua awali Ili kuwajengea watoto hofu ya Mungu kuepukana na makundi mabaya kama panya road..hayo amesema walipokuwa wakikabidhi hijabu kwa mabinti wa kiislam.
AkiitambulishaTaasisi ya mama ongea na mwanao Yvonne cherrie Maarufu kwa jina la Mona Lisa amesema taasisi inajishughulisha na mambo mbalimbali ya kijamii ,utamaduni, afya na siasa pia huku akidhihirisha kuwa bado wanatamani wadau wengi wajitokeze Ili kuweza kuwafikia watoto wengi zaidi katika kampeni ya Samia nivishe viatu ambapo katika zoezi hili wameshirikiana na Mamlaka ya Bandari (TPA) na Barron Shoes ambao ni watengenezaji, wasambazaji na wauzaji wa viatu walivyovigawa shuleni hapo vikiwa ni maalum kwa wanafunzi pekee.
Nae Mkurugenzi na Mwanzilishi wa viatu vya Barron (Barron shoes) Jack Kawishe amesema viatu vyao ni vigumu vizuri na imara vinavyotengenezwa na malighafi halisi ya kitanzania na kuunzwa ndani ya nchi..
Mwisho, Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti inaishukuru sana taasisi ya Mama ongea na mwanao pamoja na kundi zima la wasanii kwa majitoleo yao makubwa na kwa kugusa maisha ya watoto wa kitanzania wenye hali duni kimaisha ili kuweza kuwaongezea hamasa na hari ya kupenda shule.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.