Tarehe 15.02.2023 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya kibiti iliyopo kitongoji cha lumiozi kata kibiti kulifanyika mafunzo ya watumishi wa ajira za mwaka 2021-2022. Mafunzo hayo yalioongozwa na Afisa utumishi Msena Bina na nakuwezeshwa na Afisa tehama wilaya Eng. Jeta Mfaume.
Lengo la mafunzo hayo ni kutoa Elimu elekezi ya awali kwa watumishi wapya kazini pamoja na Madiwani pindi watakapoingia madarakani ( induction course ) kwa njia ya mtandao.
Aidha baada ya kuhitimu mafunzo hayo kila mtumishi husika atafanya mtihani online, na mtihani huo utakuwa moja ya kigezo cha kuthibitishwa kazini.
“Nataka wote tusikilize kwa makini wakati mwezeshaji akiendelea na mafunzo ili kupata uelewa wa pamoja ili yeyote kati yenu akashindwa kuthibitishwa kazini kwa sababu ya kufeli mtihani utakao fanyika mwishoni mwa mafunzo hayo” alisema Msena Bina.
Vilevile Afisa utumishi amewataka watumishi hao kuwa makini na kuhakikisha wote wanajisajili kwenye mfumo sambamba na kufanya mafunzo hayo na mwisho kuhakikisha wanawasilisha vyeti vya kuhitimu mafunzo hayo ili hatua za kuthibitisha watumishi kazini ziendelee. Pia amewataka watakapokuwa wanajifunza kuhakikisha wanaelewa vizuri ili isitokee Mtumishi kushindwa kujua taratibu na kanuni za utumishi wa Umma.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.