“Watumishi wenzangu naomba tuwe wasikivu kwenye mafunzo haya ya mfumo unaopima utendaji wetu wa kazi na tujitahidi kuzingatia maelekezo, kwasababu ukisikia vibaya au ukasikia ndivyo-sivyo ndivyo unavyokwenda kuathiri kazi yako na ya wale walio chini yetu”. Maneno hayo yamesemwa leo tarehe 24 Nov. 2023 na Bw. Zakayo Mlenduka ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti
wakati akifungua mafunzo ya kutumia mfumo wa kutathmini na kuhakiki utendaji kazi wa Watumishi na Taasisi (PEPMIS) yaliyotolewa kwa wakuu wa Idara waliopo Halmashauri ya wilaya ya Kibiti.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.