Waziri wa TAMISEMI Ofisi ya Rais Mhe.Mohamed Mchengerwa amewaagiza Viongozi wa ngazi zote Wilaya ya Kibiti kufanya kazi kwa kuwasililiza wananchi kupitika vikao na mikutano kuanzia Kitongoji hadi Wilaya kwani watanzania wamewaamini hivyo wanapaswa kuwatumikia wananchi.
"Endelezeni tabia ya kuwasililiza wananchi katika maeneo yao, shukeni huko chini mkawasikilize mjue kero na changamoto zao" Alisema Mhe. Mchengerwa.
Vilevile amewasisitiza Viongozi hao kufanya kazi kwa kugawana majukumu na mwisho wa siku kuja na mjumuiko utakaochanganua changamoto zilizopo na kuzipitia suluhisho kwa wakati
" Nimeweka utaratibu mpya wa kupeana taarifa, tarehe 16 ya kila mwezi tutapokea taarifa kutoka Wilaya zote, na hii itatusaidia kujipima tuone namna ya kutatua kero za wananchi." Alisema Mhe. Mchengerwa.
Hata hivyo Waziri huyo wa TAMISEMI amebainisha kuwa kuna kila sababu ya kuifungua kibiti na Pwani kwa ujumla kwa kuhakikisha Wilaya zilizopo nyuma zinapiga hatua na zilizopo mbele zinaendelea zaidi na kujikwamua kimaendeleo.
Akikagua ujenzi wa shule mpya ya msingi Bungu unaotekelezwa na mradi wa Boost Waziri Mchengerwa ameagiza majenzi yote kukamilika kwa wakati kwani miradi yote haitakuwa na muda wa nyongeza huku akikiri kuridhiwa na ujenzi huo.
Mbali na hayo amesisitiza uimrishwaji wa mahusiano mazuri ya Chama Tawala na Serikali kwani ilani ya Chama lazima itekelezwe kupitia Serikali iliyopo madarani hivyo ni suala lisiloepukika, lazima kazi ifanywe Kwa kushirikiana.
Mwisho Waziri amesema changamoto, kero zote amezipokea na ameahidi kuzifanyia kazi huku akimwagiza Meneja wa Tarura Wilaya ya Kibiti kuhakikisha kipande cha barabara ya km 2.3 kutoka Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti mpaka barabara kuu kinakamilika kwa kiwango cha lami kabla ya 2025.
Katika ziara hiyo Viongozi Chama na Serikali Wilaya ya Kibiti kwa nyakati tofauti wameshukuru ujio wa Kiongozi huyo aidha wamempongeza Rais wa jamhuri ya Tanzania kwa kazi nzuri anayoifanya katika utekelezaji wa maendeleo Wilayani Kibiti.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.