Waziri wa Elimu Mhe. Joyce Ndalichako (MB) akikagua miradi ya miundombinu ya Elimu leo Wilayani Kibiti,katika ziara aliyoifanya ya kutembelea miradi mbalimbali.
Katika ziara hiyo Mhe. Waziri ametembelea Shule ya msingi Kiomboni ambapo alikutana na madarasa yaliyochakaa na Kuahidi awamu ya pili ya fedha za Miradi zitakazoelekezwa Wilayani Kibiti Shule hiyo itapewa kiupambele cha kwanza.
Sambamba na hilo Mhe.Waziri ameweka mawe ya msingi na uzinduzi kwa baadhi ya miradi katika Shule za msingi na Sekondari.Shule ya Sekondari Nyamisati iliyopo Kata ya Salale imewekewa jiwe la msingi katika mabweni mawili,la wasichana na wavulana yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 64 kwa kila moja.
Aidha Mhe. Waziri amekagua nyumba mbili za walimu zilizojengwa katika Shule hiyo, na kupongeza uongozi wa Wilaya kwa kusimamia vizuri pesa za serikali kwa kujenga majengo mazuri kwa gharama ndogo.
"Ndugu zangu wa Salale ninawaomba Miundombinu hii ya Elimu ikatumike kuboresha na kuinua kiwango cha Ufaulu, kwani Walimu wetu wamepata nyumba za kuishi karibu, na wanafunzi wetu wamepata mabweni ili yawasaidie kutokana na umbali wa wanakotoka.Basi ndugu zangu hii ikawe chachu ya kuinua kiwango cha Ufaulu kwani mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji umeboreshwa. Hili ni deni kwenu watu wa Salale."Amesema Waziri.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.