8.12. 2023.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Bw Hemed Magaro amefungua mafunzo ya ukusanyaji wa takwimu za vyoo Bora kwa Wenyeviti wa Vitongoji na Maafisa Afya wa Kata Wilayani Kibiti katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.
"Ukiwa kama Mwenyekititi wa Kitongoji wewe ndiyo kiongozi katika Kitongoji chako, tunataka kujua (takwimu) idadi ya vyoo Bora vilivyopo" Alisema Magaro.
Katika Ufunguzi huo Mkurugenzi Magaro aliwasisitiza Wenyeviti hao kuhakikisha kaya zote zinaboresha vyoo ili kukabiliana na magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu ambayo yameshaanza kwenye Mikoa ya Kagera na Kilimanjaro.
"Kipindupindu ni uchafu, tukizingatia usafi na kuwa na vyoo Bora hatuwezi kupatwa na magonjwa ya mlipuko kasimamieni hilo kwa weledi, tunatakiwa kuwa na tahadhari " Alisema Magaro.
Aidha Mkurugenzi huyo mbali na zoezi la ukusanyaji takwimu za vyoo Bora amewaagiza Maafisa Afya kupitia Kata zao kwa kushirikiana na Wenyeviti wa Vitongoji kusisitiza wanajamii umuhimu wa kuwa na vyoo.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.