Tarehe 31/01/2022, Kamati ya fedha,Uongozi na mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti, kwa robo ya pili mwaka wa fedha 2022/2023 imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwenye Halmashauri ambapo walitembelea miradi minne iliyojikita katika idara ya Elimu na Afya.
Katika ziara hiyo iliyoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Omari Twanga kukagua miradi ya ujenzi wa Kituo cha afya Nyamatanga, Zahanati Nyambagala, jengo la upasuaji Kibiti na ujenzi wa nyumba 4 za Walimu Kata ya Bungu kutoka vyanzo vya Mapato mbalimbali.
Wakiwa katika Kata ya Ruaruke ambako ujenzi wa kituo cha Afya Nyamatanga kilipokea fedha za TASAF jumla ya sh.446,006,356.18 kwa ajili ya ujenzi wa maabara, jengo la upasuaji, jengo la kuhifadhia maiti Pamoja na ukarabati wa jengo la OPD.
Vile vile kamati imefanikiwa kukagua mradi wa ujenzi wa wodi ya upasuaji katika Kituo cha afya kibiti wenye thamani ya sh.mil 124,500,000,00.kwa ufadhili wa KOFFIH International na ujenzi upo katika hatua ya kupiga plasta na katika kata ya Dimani ujenzi wa zahanati ya Nyambagala wenye thamani ya sh.72,000,000 kwa fedha za mapato ya ndani na Ujenzi upo hatua ya umaliziaji wakati ujenzi wa nyumba 4 za Walimu katika Shule ya Msingi Pagae wenye thamani ya sh. 100,000,000 kwa fedha za Taasisi ya Elimu Tanzania (TEA) ujenzi upo katika hatua ya boma.
Katika hatua nyingine kamati imeazimia kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais Dr. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za mradi wa TASAF,Kamati imesisitiza fedha hizo zilizotolewa zitumike kama ilivyoelekezwa, pia kamati imewapongeza wananchi kwa juhudi za kujitolea katika vijiji vyote ambako miradi inatekelezwa, kamati imeshauri wananchi kujiunga na bima za afya za ICHF kwa ajili ya kurahisisha huduma .
Aidha katika ziara hiyo kamati imeagiza kufunga gata za kukingia maji katika mradi wa kituo cha afya Nyambangala ikiwa ni pamoja kuhakikisha malipo ya mzabuni yanafanyika mapema kwa kufuata taratibu za manunuzi na vifaa kufikishwa kwa wakati .
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.