Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Ndg. Mohamed I. Mavura amekua na mwendelezo wa ziara za ukaguzi wa miradi inayotekelezwa na fedha za Serikali Kuu baada ya kupokea Tsh 420,000,000 kwa ajili ya vyumba 21 vya madarasa katika shule za Sekondari kwa mwaka wa masomo 2023.
Akiwa katika shule za Sekondari za Dimani, Mtawanya, Nyambili Nyambunda na Mwambao kwa nyakati tofauti Mavura amezipongeza kamati za majenzi kwa kasi na kazi nzuri zinazoendelea kuelekea hatua ya upauaji .
Bw. Mavura ameiagiza Idara ya manunuzi kukamilisha manunuzi na kufikisha vifaa vya Ujenzi kwa wakati Ili kuendana na kasi ya majenzi inayoendelea katika miradi hiyo lengo likiwa ni kukamilisha kazi kwa wakati . Pia akazihimiza kamati za majenzi kufuata maelekezo kutoka idara ya manunuzi na si vinginevyo kwani wakienda kinyume na maelekezo mapungufu yoyote yatakayijitokeza watahusika kufidia .
Vilevile Mavura amezisisitiza kamati za majenzi kuhakikisha zina mawasiliano ya karibu ili kutambua mapungufu na uhitaji wa vifaa vilivyosalia katika shule ambazo zimeshamaliza ujenzi kwa kuuziana au kuazimishana vifaa ili kuepuka kuanza kutafuta sehemu nyingine kwa gharama za juu.
“Kuna vifaa kama vile mchanga,kokoto,mbao za rinta hakuna haja ya kuanza kutafuta sehemu nyingine ni jambo la mawasiliano baina ya shule kwa shule Pamoja na idara ya manunuzi kwani sisi sote ni wajenzi wa nyumba moja”alisema Mavura.
Aidhaa Afisa Elimu Sekondari Anna Shitindi akiwa katika Sekondari ya Nyambili Nyambunda inayojenga tundu 12 za vyoo zenye thamani ya sh 12,000,000, kwa fedha za mapato ya amesisitiza Ujenzi huo kwenda sambamba na vyumba madarasa ili kusaidia kupata usajili wa shule kwa haraka pindi ukaguzi utakapofanyika.
Katika ziara hiyo Mkurugenzi aliambatana Afisa Elimu Sekondari Anna Shitindi Afisa Manunuzi ,Rose Kahembe na Maafisa mipango Naomi Maendaenda na Maulid Ndungutu.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.