Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mh. Abubakar Kunenge amefanya ziara wilayani kibiti Leo tarehe 07.11.2023, ambapo amekagua na kupokea taarifa za utekelezaji wa miradi 6 ambayo ni Mradi wa maji Mjawa, Mradi wa maji Jaribu Mpakani, Ujenzi wa shule mpya ya sekondari Jaribu, Ujenzi wa shule ya Msingi Bungu, Ujenzi wa shule ya sekondari Lumyonzi pamoja na Ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Kibiti.
Mh. Kunenge amewapongeza wananchi kwa ushirikiano wao katika kufanikisha miradi hiyo pia amewasisitiza wananchi kuitumia vyema miradi waliyopata kwa maendeleo ya Taifa.
Aidha, Mkuu wa Mkoa amefanya Mkutano wa hadhara na Wananchi wa Kibiti ambapo amesikiliza na kujibu kero zao na zile zilizohiaji ufuatiliaji amezichukua na kuahidi kuzifanyia kazi kwa haraka.
Copyright ©DED-KIBITI 2017 . All rights reserved.